Pata taarifa kuu

Kisiwa cha Reunion kimefungwa kutokana na tishio la tufani kubwa ya kihistoria

Mkuu wa mkoa wa idara ya Ufaransa iliyoko katika Bahari ya Hindi ametangaza kuwepo kwa tahadhari ya zambarau, kiwango cha juu zaidi, Jumatatu Januari 15 kuanzia nane usiku Jumatatu, kwa kuwasili kwa kimbunga Belal.

Mawimbi makubwa yanapasuka kwenye ukingo wa Kisiwa cha Reunion, ikikaribia tufani Belal, Jumapili Januari 14.
Mawimbi makubwa yanapasuka kwenye ukingo wa Kisiwa cha Reunion, ikikaribia tufani Belal, Jumapili Januari 14. AFP - RICHARD BOUHET
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa hali ya wasiwasi itaanza kuongezeka katika kisiwa cha Reunion, wakaazi wengi bado wamechukua fursa ya saa za mwisho za utulivu siku ya Jumapili kwenda matembezini. Ugavi wa chakula na maji umemefanyika, lakini wachache wao wamefunga nyumba zao. Wengine hata wanatilia shaka vurugu za tukio hilo na kusema kuwa hawachukulii tahadhari maalum. "Tunachopaswa kufanya sasa ni kusubiri," mkazi mmoja, Lola Fourmy alimwambia mwandishi wetu katika kisiwa hicho, Jumapili saa sita mchana, wakati akiangalia anga ikiwa katika rangi ya kijivu.

Hata hivyo, maagizo kutoka kwa mamlaka ni makali. Kuanzia siku ya Jumapili jioni hadi Jumanne asubuhi, "kila mmoja na kila mtu lazima ajifungie mahali salama," amsema gavana Jérôme Filippini wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Mwakilishi wa serikali katika Reunion ametoa wito kwa wakazi takriban 870,000 wa kisiwa hicho "kujitolea saa zinazokuja bila kufanya lolote isipokuwa kujiandaa kwa kusalia nyumbani", hasa kwa kuhakikisha "mahali pa kujihifadhi' na 'upatikanaji wa hifadhi [zao]'.

Kitengo cha mgogoro

Katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandaoa wa X (zamani ikiitwa Twitter) waziri wa Mambo ya Ndani na masuala ya ng'ambo Gérald Darmanin ametoa wito kwa wakazi wa Réunion kwa "kusalia nyumbani kwao na kutotembea". "Mambo yote yamewekwa sawa" kwa kuweza kuwasaidia, ameongeza, na kuhakikisha kwamba anafuatilia hali inavyoendelea "kwa karibu", kwa kushirikiana na Rais Emmanuel Macron na Waziri Mkuu Gabriel Attal, ambaye aliitisha kitengo cha mgogoro katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Katika mtandao huo wa kijamii, rais wa eneo hilo Huguette Bello amewaalika "wakazi wa Reunion kuchukua tahadhari kubwa". "Mtihani mkali unatukabili," amesema.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.