Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: ICC yatoa waranti mbili za kukamatwa kwa maafisa wa Urusi

Luteni Sergei Kobylach na Admiral Viktor Sokolov, kamanda wa kikosi cha wanamaji katika Bahari Nyeusi, wanashukiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Ukraine kati ya mwezi Oktoba 2022 na mwezi Machi 2023. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekaribisha hatua hii mpya iliyochukuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ili haki itendeke.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini Hague, Uholanzi.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini Hague, Uholanzi. AP - Mike Corder
Matangazo ya kibiashara

Maudhui ya waranti hizi za kukamatwa mara kwa mara ni siri, anaelezea mwandishi wa RFI huko Hague, Stéphanie Maupas. Majaji wameweka wazi uwepo wao, kwa lengo moja: kusaidia kuzuia uhalifu kama huo. Hivi ndivyo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inaeleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Hata hivyo inajulikana kwamba mwendesha mashtaka anawashutumu maafisa hao wawili wa uhalifu wa kivita kwa shambulio la miundombinu ya kiraia, mashambulizi yaliyoelekezwa hasa dhidi ya mitambo ya kuzalisha umeme na vituo vya umeme vilivyoathiriwa chini ya amri ya maafisa hao wawili; na kwa mujibu wa majaji, mashambulizi haya yalisababisha uharibifu mkubwa kwa upande wa raia.

Ni kampeni ya mzshambulizi ambayo iliathiri Ukraine nzima, kati ya "angalau Oktoba 10, 2022 na angalau Machi 9, 2023", inathibitisha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, na ambayo inaweza kuwa sehemu ya sera ya Serikali inayohusisha mashambulizi yanayolenga raia. Na kwa hivyo, maafisa hao wawili wanashukiwa kufanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa vitendo vilivyosababisha "mashambulio makubwa dhidi ya uadilifu wa mwili au kiakili".

Waranti hizi za kukamatwa ni pamoja na zile zilizotolewa mwaka mmoja uliopita dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na Kamishna wake wa Haki za Watoto, Maria Lvova-Belova.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.