Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Angalau kumi wajeruhiwa baada ya mashambulizi ya Urusi katikati ya Kiev

Milipuko imesikika Alhamisi Machi 21 katikati mwa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, baada ya tahadhari ya anga kwa makombora na ndege zisizo na rubani , na kusababisha watu kumi kujeruhiwa, siku moja baada ya vifo vya raia kadhaa huko Ukraine na Urusi kila upande wa mpaka wa pamoja.

Wazima moto wakiwa kazini baada ya shambulio katikati mwa Kyiv, Machi 21, 2024.
Wazima moto wakiwa kazini baada ya shambulio katikati mwa Kyiv, Machi 21, 2024. AP - Vadim Ghirda
Matangazo ya kibiashara

Takriban milipuko mikubwa kumi ilisikika asubuhi na mapema katika mji mkuu wa Ukraine, pamoja na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani. Kwenye mitandao ya kijamii, picha zilionyesha wakaazi wakikimbilia kwenye vyumba vya chini na vituo vya metro.

Kwenye Telegram, meya wa mji wa Kyiv, Vitali Klitschko, ameripoti majeruhi kumi. Pia alizungumza juu ya "mabaki ya roketi" yaliyoanguka katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu, haswa kwenye "jengo la makazi". Jeshi la Wanahewa linasema liliharibu makombora 31, yakiwemo makombora mawili ya balistiki ya Kinzhal usiku kucha.

Mashambulio ya anga na uvamizi pande zote mbili za mpaka

Mashambulizi makubwa ya hivi karibuni  ya Urusi dhidi ya Kiev yalifanyika mwishoni mwa mwezi Januari 2024. Siku ya Jumatano, Ukraine na Urusi ziliripoti mashambulizi ambayo yalisababisha vifo vya raia kadhaa kila upande wa mpaka wao wa pamoja, ambapo milipuko ya mabomu iliongezeka hivi karibuni.

Katika Kharkiv, mji wa pili wa Ukraine, takriban watu wanne waliuawa na saba kujeruhiwa katika shambulizi la Urusi mchana kweupe, gavana wa jimbo hilo Oleg Synegubov alitangaza. Mwili mmoja uliweza kuondolewa na nyinginemiwili kubaki imenaswa chini ya kifusi, aliongeza, huku akisema watu wawili waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya. Kharkiv ambayo inapatikana karibu kilomita arobaini kutoka mpaka na Urusi, ambayo ilikuwa na karibu wakaazi milioni 1.5 kabla ya uvamizi wa Urusi miaka miwili iliyopita, inashambuliwa mara kwa mara na jeshi la Urusi.

Takriban kilomita 70 kutoka eneo la Belgorod nchini Urusi, watu watatu walikufa na wanne walijeruhiwa katika msururu wa milipuko ya mabomu, haswa "mengi" katika moja ya wilaya za mpaka, gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov alisema. Tangu Jumatano asubuhi, eneo hilo limekuwa chini ya "mashambulio makubwa ya mabomu", hasa roketi nyingi, alisema, akimaanisha wilaya ya mpaka inayolengwa na mashambulizi ya anga na uvamizi wa ardhini wa makundi yenye silaha yanayotoka 'Ukraine. Majengo ya makazi, shule na shule mbili za chekechea pia ziliharibiwa, kulingana na gavana. Hakukuwa na wanafunzi wala walimu, mamlaka za mkoa zimeamua wiki hii kufunga shule kwa muda katika maeneo ya mpakani kutokana na hatari ya mashambulizi.

Mjini Kiev ambako alikuwa katika ziara rasmi, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan kwa upande wake alitangaza kuwa hawezi kutabiri kama na lini Congress itapitisha mpango wa msaada wa kijeshi wa dola bilioni 60 kwa Ukraine, ambao bado umezuiwa katika Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Republican.

Siku ya Alhamisi, Australia imetangaza kuwa inajiunga na muungano wa kimataifa wa ndege zisizo na rubani kusaidia juhudi za vita vya Ukraine, zinazoongozwa na Uingereza na Latvia. Ukraine inatumia sana ndege zisizo na rubani kufidia uhaba wake wa makombora ya mizinga. Tangu kuanza kwa mzozo mnamo 2022, mamia ya maelfu ya vifaa hivi vimetumiwa na Kyiv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.