Pata taarifa kuu

Shambulio jipya la Urusi lalenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine

Nchini Ukraine, wanajeshi waliojihami wameripotiwa kushambulia vituo viwili vya kusafisha mafuta na kambi ya jeshi la anga katika eneo la Krasnodar usiku wa Ijumaa, huku Waukraine wakikumbwa na shambulio jipya la makombora ya Urusi usiku wa jaan kuamkia Jumamosi.

Baada ya mashambulio ya Urusi katikamji wa Kyiv, Aprili 25, 2024 (picha ya kielelezo).
Baada ya mashambulio ya Urusi katikamji wa Kyiv, Aprili 25, 2024 (picha ya kielelezo). AP - Vadim Ghirda
Matangazo ya kibiashara

Wakati Urusi ikiendelea na mpango wake wa kuharibu miundombinu ya nishati ya Ukraine, anaandika mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze, shambulio la jana usiku linaonyesha kuwa Ukraine bado haina uwezo wa kutosha kulinda eneo lake lote.

Mitambo minne ya nguvu ya mafuta yaathiriwa

Kati ya makombora 34 ya Urusi yaliyorushwa, 21 pekee ndiyo yalinaswa, mengine yaliangukia kwenye angalau mitambo minne ya kuzalisha umeme wa joto pamoja na hospitali ya wagonjwa wa akili mjini Kharkiv jana usiku. Mtu mmoja alifariki, kumi na wanne walijeruhiwa wakati wa shambulio hili, baada ya hapo Rais Zelensky alikumbusha hitaji la dharura la Ukraine kupokea mifumo zaidi ya ulinzi wa anga. Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk, aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP, alibainisha kwenye X (zamani Twitter) kwamba moja ya makombora yaliyorushwa na Urusi wakati wa usiku ilianguka huko Ukraine "kilomita 15" kutoka mpaka wa Poland.

Shambulio la masafa marefu kwenye vituo viwili vya kusafisha mafuta vya Urusi

Kwa upande wake, Kyiv, kulingana na chanzo cha kijasusi, ilizindua droni za masafa marefu dhidi ya vinu viwili vya kusafisha mafuta na kituo cha jeshi la anga katika mkoa wa Krasnodar (Urusi), na kusababisha moto na kukatizwa kwa shughuli katika angalau moja ya mitambo ya kusafisha mafuta, kulingana na afisa mmoja wa Urusi. Mashambulizi haya yana umuhimu wa kimkakati kwa kyiv kwani yanaathiri malengo ya kijeshi ambayo yanaunga mkono juhudi za vita vya Urusi. Wizara ya Ulinzi ya Urusi, iliyonukuliwa na shirikala habari la AFP, ilitangaza mapema Jumamosi kwamba ndege zisizo na rubani 68 za Ukraine zilinaswa usiku mmoja, zikiwemo 66 katika eneo la Krasnodar na nyingine mbili katika peninsula ya Crimea, iliyotwaliwa mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.