Pata taarifa kuu
UFARANSA

Sarkozy atangaza kuwania tena urais nchini Ufaransa

Katika kile kinachoonekana kukaribia kwa uchaguzi mkuu wa rais Nchini Ufaransa, hatimaye rais Nikolas Sarkozy ametangaza rasmi kuwania tena muhula wa pili wa urais.

AFP PHOTO / THOMAS COEX
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia kituo kimoja cha televisheni nchini Ufaransa, rais Sarkozy amesema ametangaza nia yake hiyo huku akijiamini kuwa ataibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa nne na watano.

Licha ya kuonekana kuungwa mkono na wananchi wengi kiongozi huyo anatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa chama cha Socialist Francois Hollande.

Hatua hiyo ya Sarkozy imeibua maswali kama atafanikiwa kutetea kiti chake kwani mgombea Francois Hollande anaonekana kuleta upinzani mkubwa wa kisiasa ingawaje watu wengine wanampa nafasi Sarkozy kwa madai kuwa ameijengea sifa Ufaransa ndani na nje ya Bara la Ulaya.

Hata hivyo wananchi wenye dhamana ya kupiga kura ndiyo wana jukumu la kuamua kiongozi yupi watakayemchagua kwa matakwa yao huku wakiweka mbele maslahi ya taifa lao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.