Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-UKRAINE-Machafuko

Marekani yaionya Urusi kuhusu Ukraine

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden ameionya Urusi kwa kile alichokiita kuingilia masuala ya ndani ya Ukraine na kutaka kuigawa nchi hio baada ya kuunga mkono wanaharakati wanaounga mkono wa kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.

Makamu wa rais, Joe Biden (kushoto) akiwa pamoja na waziri mkuu wa Ukraine Arseny Yatseniuk mbele ya vyombo vya habari mjini Kiev, aprili 22 mwaka 2014.
Makamu wa rais, Joe Biden (kushoto) akiwa pamoja na waziri mkuu wa Ukraine Arseny Yatseniuk mbele ya vyombo vya habari mjini Kiev, aprili 22 mwaka 2014. REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wanaounga mkuno kujitenga kwa jimbo la Cremia wakivukabaadhi ya maeneo ya hatari ya Saint-Georges, aprili 22 mwaka 2014.
Wanaharakati wanaounga mkuno kujitenga kwa jimbo la Cremia wakivukabaadhi ya maeneo ya hatari ya Saint-Georges, aprili 22 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich

Kwa upande wake kaimu rais wa Ukraine Olexandre Tourtchinov amebaini kwamba wanaharakati wanaounga mkono wa kujitenga, wamevuka “eneo la hatari”, na kutangaza kuanzisha kwa mara nyingine operesheni “dhidi ya ugaidi” mashariki mwa taifa hilo, operesheni ambayo ilisitishwa kabla ya pasaka, baada ya kugundua miili ya watu wawili waliyouawa, ambapo mmoja miongoni mwa watu hao anasadikiwa kuwa mbunge wa jimbo kutoka chama cha Ioulia Timochenko, Batkivchtchina.

 

Kwa mujibu wa Tourtchinov, matumaini ya kupatikana kwa amani baada ya kutia saini makubaliano ya kimataifa mjini Geneva alhamisi iliyopita yameonekana kufifia, baada ya wanaharakati wanaounga mkono kujitenga “kudhibiti jimbo la Donetsk”.

Akikamilisha ziara yake Joe Biden ameionya nchi ya urusi kuacha mara moja vitendo vya kuingilia masuala ya ndani ya nchi ya Ukraine kwani haina haki ya kufanya hivyo.

Kauli hiyo ya Joe Biden imekuja wakati huu urusi ikiwa na maelfu ya wanajeshi wake kwenye mpaka wake upande wa mashariki mwa Ukraine hatua ambayo inapingwa vikali na jumuiya ya kimataifa.

Biden amesisitiza kuwa Marekani na washirika wake kamwe hawatarusu Urusi kuingilia Ukraine katika mambo yake ya ndani kwani ni kinyume na sheria za kimataifa.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry alimuelezea jana mwenyeji wake wa Urusi Sergueï Lavrov wasiwasi wake juu ya ukosefu wa hatua madhubuti ambazo zinapaswa kuchukuliwa na Urusi ili kurejesha hali ya utulivu nchini Ukraine.

Katika hatua nyingine Marekani ambayo inaituhumu Urusi kuendelea kuchochea vurugu nchini Ukraine, imetangaza kutuma wanajeshi 600 kwa ajili ya mazoezi ya kijeshi katika nchi jirani ya Poland, na imeahidi kuiwekea Urusi vikwazo zaidi.

“Muda umewadia sasa kuachana na maneno na kuanza kutekeleza vitendo (…) Tunapaswa kujadili hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa haraka, muda umehesabiwa”, Biden amesema akisisitiza akiwa pamoja na waziri mkuu wa Ukraine Arseni Iatseniouk walipokua wakitoa tangazo mbele ya vyombo vya habari mjini Kiev.

Wanaharakati wanaounga mkuno kujitenga kwa jimbo la Cremia  wakijificha nyuso.
Wanaharakati wanaounga mkuno kujitenga kwa jimbo la Cremia wakijificha nyuso. REUTERS/Baz Ratner

Biden ameitaka Moscow kuyaondoa majeshi yake yanayoendelea kukusanyika kwenye mpaka, na kuacha kuunga mkono watu wanaojificha nyuso na kuvaa sare zisiyokua na ishara yoyote ya jeshi.

Biden ameionya Urusi kwamba iwapo itaendelea na chokochoko zake, itachukuliwa hatua kali ikiwemo kutengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.