Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Machafuko

Mzozo wa Ukraine;waasi wa mashariki kupiga kura ya maoni ya kujitenga au kubaki na Ukraine

Watu wanaounga mkono Urusi katika majimbo mawili ya mashariki mwa Ukraine wanapiga kura ya maoni hatua ambayo mataifa ya magharibi na serikali ya kiev imeilaani.

Maandalizi ya kura maoni mashariki mwa Ukraine yametimia
Maandalizi ya kura maoni mashariki mwa Ukraine yametimia AFP PHOTO / GENYA SAVILOV
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa harakati hizo huko Donensk na Luhansk wanaendelea na upigaji kura licha ya raisi wa Urusi Vladimir Putin kutoa wito wa kuahirisha.

Serikali ya Ukraine imesema kuwa kura hiyo itasababisha maeneo hayo kujiharibu yenyewe.

Hata hivyo watu wanaomiliki silaha wanaounga mkono Urusi na kudhibiti majengo ya serikali katika miji kadhaa wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa Ukraine.

Ripoti zinasema kumekuwa na makabiliano makali usiku kucha katika viunga vya mji unaoshikiliwa na waasi Sloviansk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.