Pata taarifa kuu
Ukraine-Usalama

Rais wa Ukraine akataa kuongeza muda wa kusitisha mapigano

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko anayeungwa mkono na nchi za Magharibi ametangaza serikali yake kutoongeza muda wa kusitisha mapigano kati yake na waasi wa mashariki mwa nchi hiyo na badala yake anasema vikosi vyake vitakomboa miji hiyo.

Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akionya wanaharakati wanaoshikilia maeneo ya mashariki mwa Ukraine.
Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akionya wanaharakati wanaoshikilia maeneo ya mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Olivier Hoslet
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, rais Poroshenko amewaambia wananchi wake kuwa baada ya kupitia kwa kina hali ilivyo kwasasa mashariki mwa nchi hiyo yeye kama amiri jeshi mkuu ameamua kutoongeza muda wa makataa ya kusitisha mapigano na wapiganaji hao wenye silaha.

Tangazo la rais Porosheko linatishia kuzorota kwa usalama zaidi mashariki mwa nchi hiyo na pia kukwamisha juhudi za Ujerumani na Ufaransa ambazo ziliomba utawala wa Kiev kuongeza muda wa makataa hiyo bila mafanikio.

Rais Poroshenko amesisitiza kuwa serikali yake iko tayari kusitisha mapigano muda wowote kuanzia sasa na kwamba atafanya hivyo iwapo tu pande zinazohusika kwenye mzozo huo zitaonesha utayari wao wa kushiriki mazungumzo na kusaini mkataba wa amani.

Wachambuzi wa mambo walitabiri hili kutokea kutokana na shinikizo ambalo rais Poroshenko analipata toka kwa wananchi wa taifa hilo ambao wanataka awe na msimamo mkali kuhusu wapiganaji waliochukua baadhi ya miji ya mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.