Pata taarifa kuu
URUSI-MALAYSIA-UKRAINE-Uchunguzi

Urusi yahitaji kushiriki katika uchunguzi

Urusi imesema iko tayari kutoa mchango wake kwa kusaidia kwa uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia Airlines yenye chapa MH17 iliyodunguliwa mashariki mwa Ukraine ikiwa na abiria 283, hususan kuwatuma wataalamu wake kwenye eneo la tukio.  

Rais wa Urusi, Vladimir Putine, akipongeza azimio la Umoja wa mataifa.
Rais wa Urusi, Vladimir Putine, akipongeza azimio la Umoja wa mataifa. REUTERS/Mikhail Klimetyev/RIA Novosti/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Urusi imepongeza pia azimio la Umoja wa Mataifa, linaloamuru kuweko na uhuru na nia ya kujitolea kwa kuwasili kwenye eneo la tukio kwa lengo la kuendesha uchunguzi.

“Urusi iko tayari kuwatuma wataalamu wake ili kusaidia kwa uchunguzi”, amesema waziri wa mambo ya nje wa Urusi katika tangazo aliyotoa.

“Nadhani tukio kama hili linahitaji ushirikiano wa kina wa shirikisho la kimataifa la usafiri wa ndege chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa”, ameongeza waziri wa mambo ya nje wa Urusi.

Moscow imepongeza azimio liliyochukuliwa usiku wa jumatatu kuamkia jumanne na wajumbe 15 wa Umoja wa Mataifa, Urusi ikiwemo, amabalo linalani shambulizi dhidi ya ndege ya Malaysia Airlines yenye chapa MH17, na kuamuru usalama uimarishwe kwenye eneo la tukio ili uchunguzi ufanyike kwa uhuru.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Urusi amesema pia kwamba ingelikua bora zaidi azimio hilo la Umoja wa Mataifa lishawishi pande husika katika mgogoro unaoendelea nchini Ukraine kusitisha mapigano hasa katika eneo la tukio na kurahisishia mashiririka na wataalamu wanaoendesha uchunguzi kufika kwene eneo la tukio, hususan shirikisho la usalama na maendeleo barani Ulaya OSCE na mashirika mengine ya kimataifa.

Wakaguzi wa a shirikisho la usalama na maendeleo barani Ulaya OSCE wakati walipokua wakikagua treni inayobeba miili ya watu waliyofarika katika ajali ya ndege MH17 ya Malaysia Airlines.
Wakaguzi wa a shirikisho la usalama na maendeleo barani Ulaya OSCE wakati walipokua wakikagua treni inayobeba miili ya watu waliyofarika katika ajali ya ndege MH17 ya Malaysia Airlines. REUTERS/Maxim Zmeyev

Rais wa Urusi Vladimir Putine amepongeza usiku wa jumatatu kuamkia jumanne katika mazungumzo ya simu na mwenziye wa Uholanzi Mark Rutte kwa kuidhinisha azimio hilo. Viongozi hao wawili wamebaini kwamba kuna umuhimu wa kusitisha mapigano ili kurahisishia wataalamu kufika eneo la tukio, ikulu ya Moscow imethibitisha katika tangazo lake.

Hata hivo waasi wa Ukraine wametangaza usiku wa jumatatu kuamkia jumanne kusitisha mapigano katika eneo lenye upana wa kilomita 10 linalozunguuka eneo la tukio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.