Pata taarifa kuu
UTURUKI-Sheria-Polisi

Uturuki : maafisa 55 wa polisi wakamatwa

Viongozi wa Uturuki wamewakamata jumanne wiki hii maafisa 55 wa polisi kufuatia uchunguzi wa kina kuhusu taarifa za kashfa ya rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka vinavyoikapili polisi na sekata ya vyombo vya sheria, Televisheni za Uturuki zimetangaza.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Maafisa arobaini ambao bado wanafanya kazi na wengine ambao walistaafu wamekamatwa mjini Istanbul, akiwemo mkuu wa zamani wa kitengo cha polisi cha kupambanba dhidi ya ugaidi katika mji wa Istanbul, Omer Kose. Maafisa wengine wamekamatwa katika miji mbalimbali nchini Uturuki.

Katika operesheni hio iliyoendeshwa na polisi mapema jumanne hii asubuhi, takribani maafisa 200 wamekua wamekamatwa katika mji wa Istanbul peke yake. Televisheni za Uturuki zimeonyesha maafisa hao wakifungwa pingu mikononi. Lakini muda mchache baadae maafisa 260 wameachiwa huru.

Operesheni hio imetekelezwa katika miji 22 nchini kote Uturuki, gazeti la Uturuki la kila siku, Hurriyet limechapisha katika mtandao wake wa tovuti.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, watu hao waliokamatwa wanakabiliwa na tuhuma za ujasusi, kusikiliza simu za watu kinyume cha sheria, utumiaji mbaya wa madaraka, ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na kubuni vithibitisho visiyo halali.

Mwishoni mwa mwezi juni, utawala wa Uturuki ulianzisha uchunguzi dhidi kundi la wanadini linaloongozwa na mhubiri aliyekimbilia uhamishoni, Fethullah Gülen, ambaye ni haelewani na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.