Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-UKRAINE-MALAYSIA-Uchunguzi

Marekani: ndege ya Malaysia Airlines ilidunguliwa bila kukusudiwa

Shirika la Marekani la upelelezi FBI limeonesha baadhi ya nyaraka kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia Airlines iliyodunguliwa alhamisi juma liliyopita. Washington haitaji Urusi katika nyaraka hizo wa la mtu yeyote. Lakini wataalam hao wa shirika la Marekani la Umarekani hawakubaliane na madai ya Uruhi kwa kuituhumu kuhusika na udunguaji wa MH17.

Waasi wa Ukraine wakiwa karibu na mabaki ya ndege ya Malaysia Airlines chapa MH17, katika eneo la Donets, 22 Julai mwaka 2014.
Waasi wa Ukraine wakiwa karibu na mabaki ya ndege ya Malaysia Airlines chapa MH17, katika eneo la Donets, 22 Julai mwaka 2014. Reuters/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

Hata hivo FBI, imethibitisha kwamba Urusi imekua ikiwafadhili waasi wa Ukraine silaha hata baada ya tukio hilo la kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia Airlines. Wataalam hao wamebaini kwamba ndege ya Malaysia Airlines ilidunguliwa kwenye eneo la mazowezi ya makombora kwenye mpaka na Urusi, ambapo waasi wa Ukraine wamekua wakipata mafunzo ya kijeshi.

Picha ya namna kombora liliyorushwa angani hadi kufikia ndege imeonyeshwa kwenye nyaraka hizo. FBI imebaini kwamba iwapo wataalam wataaendesha uchunguzi kwa uhuru, bila shaka mabaki ya kombora yatapatikana kwenye eneo la tukio.

Shirika la Marekani la upelelezi lina amini kwamba ndege ya Malaysia Airlines iliunguliwa bila kukusudiwa, wakati waasi wa Ukraine walipokua wakipata mafuzo kuhusu kurusha makombora angani. Kuna uwezekano kwamba mpiganaji wa kundi hilo la waasi alikua hajapata mafunzo ya kutosha kuhusu kufyatua kombora,FBI imeendelea kusema.

Upande wa pili wa Urusi, picha za satelite zimeonyesha picha za eneo la Rostov ziliyopigwa mwaka uliyopita, na majuma ya hivi karibuni. Katika eneo hilo kunaonekana jangwa ambalo, FBI inaona kwamba ni sehemu waasi wa Ukraine wanakopata mazowezi ya kijeshi kuhusu zilaha zinazofyatua makombora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.