Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-EU-Vikwazo-Usalama

Ukraine: vikwazo vipya dhidi Moscow vyajadiliwa

Mataifa ya magharibi yamelani kitendo cha Urusi cha kuingia kijeshi nchini Ukraine, lakini yamebaini kwamba yanasubiri kuona jinsi gani hali itakavyoendelea, huku vikwazo vipya dhidi ya Urusi vikijadiliwa.

Mkuu wa sera zanje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amebaini kwamba amekua akitiwa wasiwasi na hali inayoendelea nchini Ukraine.
Mkuu wa sera zanje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amebaini kwamba amekua akitiwa wasiwasi na hali inayoendelea nchini Ukraine. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Hata hivo viongozi wa Ukraine wameombaUmoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi kuisaidi kijeshi.

Rais wa Marekani, Barack Obama na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel wamezungumza kwa simu Alhamisi wiki hii kuhusu hali inayoendelea nchini Ukraine. Viongozi hao wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuingizwa nchini Ukraine zana za kijeshi na vifaa vingine vya kijeshi, pamoja na wanajeshi wakiingia kuwasaidia waasi wa Ukraine.

Wamebaini kwamba kitendo cha Urusi cha kuchochea machafuko nchini Ukraine siyo cha kuvumilia, lazima hatua kali zichukuliwe. Lakini rais wa Marekani, ambaye amejieleza kabla ya baraza la usalama la kitaifa, amejizuia kusema kuwa kitendo cha Urusi kuingia kijeshi nchini Ukraine ni “uvamizi”, huku akitupiliambali uwezekano wa Marekani kuingia kijeshi nchini Ukraine kwa minajili ya kulisadia jeshi la taifa hilo katika mapigano dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Hata hivo wakuu wa kijeshi wa Pentagone wametangaza kwamba Marekani imekua ikianda mpango wa kuwatuma wanajeshi wake pamoja na vifaru mashariki mwa Ulaya, hususan nchini Poland na mataifa yaliyo jirani kwa lengo la kuhakikisha ushirikiano wao na mataifa ya kikanda ambayo ni wanachama wa Nato.

Barack Obama na Angela Merkel wamesema kwa sasa hakuna vikwazo vya kiuchumi vitakavyochukuliwa dhidi ya Urusi, lakini rais Barack Obama amebaini kwamba hatua kali ziko mbioni kuchiukuliwa.

Hata hivo wabunge wa Umoja wa Ulaya kutoka Uingereza na Ujerumani wamependekeza Urusi ichukuliwe vikwazo vya kiuchumi. Suala hilo ni miongoni mwa masuala yatakayogubika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika Jumamosi, Agosti 30 mwaka 2014 mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa ulaya Catherine Ashton amefahamisha kwamba amekua akitiwa wasiwasi na hali inayoendelea nchini Ukraine. Kwa upande wakw rais wa Ukraine Petro Porochenko anatazaimwa kukutana na viongozi wa taasisi za Umoja wa Ulaya kabla ya mkutano wa kilele kuanza. Balozi wa Ukraine kwenye Umoja wa Ulaya ameomba mataifa 28 wanachama wa Umoja huo kuandaa mkutano kuhusu machafuko yanayoendelea nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.