Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAQ-ISIL-Usalama

Ufaransa: François Hollande ziarani Iraq

Rais wa Ufaransa, François Hollande amejielekeza mapema ijumaa asubuhi wiki hii nchini Iraq akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje, Laurent Fabius na waziri wa ulinzi Jean Yves Le Drian. Rais Hollande ameahidi kuunga mkono serikali mpya ya Iraq.

Rais wa Ufaransa, François Hollande akipokelewa na mwenyeji wake wa Iraq, Fouad Massoum, alipowasili ijumaa Septemba 09 mjini Bagghdad.
Rais wa Ufaransa, François Hollande akipokelewa na mwenyeji wake wa Iraq, Fouad Massoum, alipowasili ijumaa Septemba 09 mjini Bagghdad. REUTERS/Ali al-Saadi
Matangazo ya kibiashara

François Hollande, amepongeza serikali ya Iraq akisema kwamba ni serkali ya mpito yenye sura ya kudumisha demokrasia nchini Iraq. Serikali hiyo mpya inaundwa na watu kutoka jamii mbalimbali iki ni pamoja na makundi hasimu, hususan watu kutoka jamii ya washia walio wengi, wasuni na wakurdi walio wachache.

Ziara hiyo ya François Hollande nchini Iraq, ni ya kwanza kwa marais wa kigeni tangu wapiganaji wakiislam waanzishe mashambulizi nchini humo Juni 09 mwaka 2014.

ziara hiyo inafanyika siku mbili baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kutangaza kupanua wigo wa mashambulizi nchini Iraq dhidi ya wapiganaji wa kiislam, na kuahidi kuwashambulia hadi nchini Syria.

Hata hivo Ufaransa ilitangaza hivi karibuni kwamba huenda ikashiriki katika operesheni ya kijeshi nchini Iraq dhidi ya wapiganaji wa kiislam, lakini ilibaini kwamba mchango wake ni wa mashambulizi ya anga pekee.

Akikutana kwa mazungumzo na rais wa Iraq, Fouad Massoum, François Hollande, amekumbusha kwamba kuna mkutano uhusuo “amani na usalama” unaoandaliwa mnamo siku mbili mjini Paris, ili kuratibu michango inayotolewa na mataifa washirika pamoja na utayari wao wa kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Dola la Kiislam. Rais wa Iraq amebaini kwamba mkutano huo ni muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.