Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Cameron kuongoza kikao cha dharura baada ya kuuliwa kwa David Haines

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameitisha kikao cha dharura cha viongozi wa juu wa usalama nchini humo, kujadili hatua ya kuchukua baada ya wapiganaji wa Kislamu wa Islamic State kumuua raia wa Uingereza David Haines kwa kumkata shingo.

David Haines kabla ya kuuliwa na wapiganaji wa Islamic State
David Haines kabla ya kuuliwa na wapiganaji wa Islamic State REUTERS/Islamic State via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kinawaleta pamoja maafisa wakuu kutoka kitengo cha jeshi na polisi nchini humo kuamua hatua haraka ya kufanya.

Mapema, Cameron alilaani mauaji hayo aliyosema ni ya kinyama na kusema kuwa Uingereza itahakikisha kuwa wauaji hao watasakwa na kuadhibiwa vikali.

Mauaji ya Haines mwenye umri wa miaka 44 na ambaye alikuwa mfanyikazi wa kujitolea nchini Syria kabla ya kutekwa nyara na wapiganaji hao, ni ya tatu dhidi ya mateka kutoka mataifa ya Magharibi ikiwa wanahabari wawili wa Marekani.

Wapiganaji hao walitoa mkanda wa video kuonesha mauaji hayo ambayo wanasema ni ujumbe kwa Uingereza kujiunga na Marekani kuwashambua katika ngome zao nchini Iraq.

Rais wa Marekani Barrack Obama amesema amesikitishwa mno na mauaji ya raia huyo wa Uingereza na kuongeza kuwa ,Marekani na washirika wake wataendelea kupambana dhidi ya wapigani hao.

Australia nayo imetangaza kuwa inatuma wanajeshi wake 600 kujiunga na wanajeshi wengine kutoka Marekani, Uingrereza na nchi za kiarabu kupambana na wapiganaji hao wa Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.