Pata taarifa kuu
UFARANSA-Siasa

Ufaransa: Manuel Valls aomba wabunge kupiga kura ya imani kwa serikali yake

Miezi mitano baada ya kupata uaminifu na Bunge la taifa, waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amekua na hofu ya kupoteza imani kwa wabunge baada ya serikali yake kutoka likizoni na kuomba wabunge wawe na imani na serikali yake.

Manuel Valls waziri mkuu wa Ufaransa.
Manuel Valls waziri mkuu wa Ufaransa. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu ambaye anatazamiwa kujieleza mbele ya Bunge jumanne alaasiri wiki hii, kabla ya kufanyika kwa kura amekua akiwasihi wabunge hasa wabunge wa chama cha kisoshalisti kuwa na imani na serikali.

Jumatatu wiki hii, Manuel Valls alifahamisha kwamba atatekeleza majukumu yake ya waziri mkuu hadi hatua ya mwisho, huku akilani maneno yaliyotumiwa na gazeti Le Monde likisema kwamba waziri huyo mkuu alitumia maneno yasikua na busara aliposema kua Septemba 7 nchini Italia kwamba Chama cha FN kinatazamiwa kuchukua madaraka.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Manuel Valls inakabiliwa na mvutano kuhusu hali ya kiuchumi inayoendelea, huku serikali hiyo ikishindwa kukabiliana na suala la ukosefu wa ajira, ambalo limekua tete.

Tafiti zinaonesha kuwa Manuel Valls amemkaribia rais François Hollande kwa kutokua na uungwaji mkono kwa raia, amabapo kwa sasa Valls ameanza kutafuta uaminifu huo kwa wabunge, wakati Katiba ya nchi hailazimishi.

Katiba ya nchi inaeleza kwamba iwapo waziri mkuu anapoteza uaminifu, anatakiwa kujiuzulu, jambo ambalo haliwezekani kwa sasa na ambalo halipawsi kupuuzwa.

Wabunge kumi na moja kutoka chama cha Kisoshalisti cha mrengo wa kushoto cha PS hawakuonesha msimamo wao katika kikako cha Aprili 8, huku wabunge kati ya 30 na 40 waliyopiga kura ya uaminifu kwa serikali kipindi hicho, wamebaini kwamba hawataonesha msimamo wao kuhusu kuwa na uaminifu au la kwa serikali ya Valls. Hata hivo wabunge wengine watatu wenye uhusiano wa karibu na kundi la wasoshalisti wamesema hawatopiga kura yoyote wakati Aprili 8 walipiga kura ya uaminifu kwa serikali.

Wakati huohuo wabunge 18 amabao ni wanaharakati wa mazingira wamesema watachukua uamzi katika dakika za mwisho kupiga kura ya ndio, kuunga mkono , kupinga au kujizuia, licha ya kuwa Aprili 8 walipiga kura ya kuwa na uwaminifu kwa serikali.

Manuel Valls atakuwa hatarini iwapo wabunge zaidi ya 15 ambao ni watetezi wa haki za binadamu watajiunga na UMP, UDI, chama cha mrengo wa kushoto na wengne ambao hawatajiorodhesha, huku idadi ya wabunge wa vyama vya mrengo wa kushoto ikiwa zaidi ya 50.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.