Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-SYRIA-EI-KOBANE-Usalama

Mkutano wa muungano dhidi ya IS: wasiwasi wa Obama kuhusu Kobane

Marekani imekutana Jumanne wiki hii na waku wa majeshi ya mataifa yanaoshiriki katika muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la Dola la Kiislam.

Barack Obama ametangaza kwamba mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam yanapaswa kuendelea.
Barack Obama ametangaza kwamba mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam yanapaswa kuendelea. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amewasihi wakuu hao kuzidisha mashambulizi katika ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam, akisema kuwa ana wasiwasi na hatma ya Kobane.

Mkuu wa majeshi yanayoshiriki katika vita hivyo, jenerali Dempsey, ambaye ameongoza mkutano huo wenye lengo la kujadili mbinu ya pamoja na jukumu la kila nchi inayoshiriki katika muungano huo wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Rais wa Marekani Barack Obama ambaye ameshiriki mkutano, ameelezea was wasi wake kuhusu hali inayojiri wakati huu katika mji wa Kobane, akibaini kwamba mji huo unakabiliwa na vitisho vya wapiganaji wa Dola la Kiislam wanaodhibiti baaadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria.

Obama amesema kwamba mashambulizi ya muungano wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la kiislam yanapashwa kuendelea, na hakuna kusubiri suluhu yoyote katika machafuko hayo.

"Kutakuwa na siku za maendeleo, na nyakati za shida", amesema Obama. Amesisitiza pia kuwa kuendesha vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislam sio tu kampeni ya kijeshi katika uwanja wa vita, bali ni vita dhidi ya ubaguzi.

Saudi Arabia na Uturuki ziliwakilishwa katika mkutano huo. Lakini kuna mvutano kati ya Washington na Ankara: Marekani inataka Uturuki ipeleke majeshi yake nchini Syria, lakini serikali ya Uturuki itafanya hivo iwapo mashambulizi ya muungano wa kimataifa yatalenga wapiganaji wa Dola la Kiislam na jeshi la Bashar Al Assad. Lakini kwa sasa, utawala wa Obama unapendekeza zaidi kuvunja kundi la Dola la Kiislam kuliko utawala wa Bashara Al Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.