Pata taarifa kuu
UFARANSA-IS-SYRIA-MAUAJI-HAKI ZA BINADAMU

Raia wa Ufaransa waendelea kujiunga na IS

Raia wa mataifa ya magharibi wameendelea kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, ambapo asilimia kati ya 20 na 25 ya wapiganaji hao ni kutoka familia zisizo za Waislam, ambao wamebadili dini na kuwa Waslam.

Mickaël dos Santos, mwanajihadi wa pili raia wa Ufaransa, ambae alitambuliwa hivi karibuni katika video kwamba amejiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Mickaël dos Santos, mwanajihadi wa pili raia wa Ufaransa, ambae alitambuliwa hivi karibuni katika video kwamba amejiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Raia wawili wa Ufaransa, Maxime Hauchard, pamoja na, Mickaël dos Santos, ndio wameshatambuliwa kuwa wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, baada ya kuonekana katika video iliyorushwa hivi karibuni. Wawili hao wana umri wa miaka 22, na walijielekeza nchini Syria mwezi Agosti, na wote ni kutoka familia zisizo za Waislam

Wadadisi wanasema raia wasio Waislam kutoka mataifa ya magharibi wamekua wakilengwa na makundi ya wapiganji wa kiislam ili waweze kushirikiana nao katika harakati zao, kwa sababu serikali zimewatelekeza raia hao.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya familia, Dounia Bouzar, makundi ya wapiganaji wa kiislam yamekua yakiwalenga wanawake, raia wa vijijini pamoja na raia wasio Waislamu , kwa sababu yanawatuhumu Waislam asilia, kuwa vibaraka vya nchi za magharibi.

Hivi karibuni kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, limemkata kichwa Peter Kassig, raia wa Marekani aliyebadili dini na kuwa muislam. Peter Kassig aliuawa baada ya kutekwa nyara nchini Syria, ambako alikua akiendesha shughuli zake za kuwahudua wakimbizi wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.