Pata taarifa kuu

Rais Erdogan aikosoa Marekani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameikosoa Marekani kuhusu vita inavyoendesha nchini Syria na Iraq dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. 

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aikoso aMarekani kwa mpango wake wa kuingilia kijeshi Syria na Iraq dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aikoso aMarekani kwa mpango wake wa kuingilia kijeshi Syria na Iraq dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Ukosoaji huo unufuata ziara ya makamu wa rais wa Marekani, Joe Biden, nchini Uturuki ambaye aliiomba Ankara kuweka wazi msimamo wake kuhusu muungano wa kimataifa dhidi ya wanajihadi, ambapo Uturuki ni mwanachama rasmi wa muungano huo, lakini haijaonyesha mpaka sasa nia ya kushirikiana na muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Jinsi muda unavyokwenda ndivyo rais wa Uturuki anavyoendelea kupoteza imani katika muungano wa kimataifa unaoongozwa na Mareakni dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Msimamo huo wa Ankara kupinga mataifa ya magharibi kuingilia kijeshi nchi za Iraq na Syria dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam si mpya. Msimamo huo wa Ankara ulionekana tangu awali kupitia visa mabilmbali. Lakini uamzi wa Marekani kuendelea kuomba Uturuki kuonesha msimamo wake katika muungano huo bila mafankio huenda ukapelekea uhusiano wa nchi hizo mbili kudorora.

Mapema mwezi Oktoba, Erdogan alituhumiwa na makamu wa rais wa Marekani kwamba Uturuki imekua ikiwaruhusu wanajihadi kutumia ardhi yake kwa kujielekeza nchini Syria na Iraq.

" Kama alisema hivo, mimi sijali", amesema rais wa Uturuki.

Novemba 22 rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na makamu wa rais wa Marekani, Joe Biden walizungumza kwa muda mrefu kuhusu jukumu la Uturuki katika muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la Dola la Kiislam.

Hata hivyo, kufuatia kauli ya Joe Biden ya kumtuhumu rais wa Uturuki, inaonekana kua Recep Tayyip Erdogan hana nia yoyote ya kushirikiana na muungano huo.

Kwa mujibu wa rais Recep Tayyip Erdogan ombi la Marekani la kutumia ngome ya jeshi la Uturuki ya Incirlik katika mashambulizi yake ya anga ambapo wanajeshi wa Marekani wamepiga kambi halikubaliki, na Marekani ina tabia ya kujifaharisha, amesema Erdogan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.