Pata taarifa kuu
UINGEREZA-MAREKANI-GUANTANAMO-SHERIA

Raia wa Uingereza wadai Aamer aachilwe huru

Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wabunge na Maseneta bila kusahau raia wa kawaida wametia saini kwenye waraka wakudai Shaker Aamer, mkaazi wa Uingereza anaye zuiliwa bila hatia tangu miaka 13 iliyopia katika jela la Marekani la Guantanamo Bay, achiliwe huru.

Mwanaharakati mmoja amevaa kama wafungwa wa Guantanamo, wakati wa maandamano ya kudai kuachiliwa huru Shaker aamer, Mei mwaka 2014, London, Uingereza.
Mwanaharakati mmoja amevaa kama wafungwa wa Guantanamo, wakati wa maandamano ya kudai kuachiliwa huru Shaker aamer, Mei mwaka 2014, London, Uingereza. CITIZENSIDE/SEE LI
Matangazo ya kibiashara

Wabunge na Masenta hao wakiwemo raia wa kawaida wamemuomba Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon kumshinikiza rais wa Marekani Barack Oboma aweze kumuachilia huru Shaker Aamer, wakati ambapo zoezi la kuwahamisha wafungwa katika jela hilo limepitishwa na serikali ya Marekani.

Shaker Aamer ni mkaazi wa mwisho wa Uingereza anayezuiliwa katika jela la Guantanamo Bay bila hatia. Shaker Aamer, baba wa watoto wanne, mwenye umri wa miaka 46, alizaliwa nchini Saudia Arabia, na alifunga ndoa na mwanamke raia wa Uingereza ambaye anaishi London.

Shaker Aamer alikamatwa nchini Afghanistan mwishoni mwa mwaka 2001 na vikosi vya Marekani, na alituhumiwa kuwa alikua akifadhili kundi la Al-Qaeda na kusajili vijana katika tawi la kundi hilo linaloendesha harakati zake nchini Uingereza.

Shaker Aamer, alipelekwa katika jela la Guantanamo Bay mwaka 2002, na ameendelea kuzuiliwa katika jela hilo, licha ya kuwa utawala wa Geroge W.Bush ulikiri mwaka 2007 kutokua na ushahidi wowote wa kuhusika kwa Shaker Aamer katika kundi la Al-Qaeda, wala jina lake haliko kwenye orodha ya majina 55 ya wafungwa ambao serikali ya Marekani imepitisha hivi karibuni kwamba wanapaswa kuhamishwa kutoka katika jela hilo na kupelekwa maeneo mengine.

Waliotia saini kwenye waraka huo ikiwa ni pamoja na zaidi ya wasanii 50, waandishi wa vitabu, wataalamu katika masuala ya sheria, Wabunge na Maseneta wa Uingereza, wamemuomba Waziri mkuu David kumpigia simu rais wa Marekani Barack Obama ili alishughulikie sula hilo la kumuachilia huru Shaker Aamer.

Watu hao waliotia saini kwenye waraka huo wamebaini kwamba Marekani ina haina nia ya kumuachilia huru Shaker Aamer kwa kuhofia kuwa ataweka bayana maovu aliyotendewa katika jela la Guantanamo Bay.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.