Pata taarifa kuu
UHISPANIA-CRISTINA-UFISADI-UTAWALA BORA

Infante Cristina afikishwa mikononi mwa Mahakama

Cristina wa Uhispania, dada wa Mfalme Philip VI, (ambaye anajulikana kwa jina la Infante Cristina), amefikishwa mikononi mwa Mahakama kwa makosa ya kodi.

Infante Cristina.
Infante Cristina. REUTERS/Daniel Aguilar/
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya familia ya kifalme, mtoto wa Mfalme anakabiliwa na makosa kama hayo, imetangaza Jumatatu hii Desemba 22, Mahakama ya Palma de Mallorca katika visiwa vya Balearic ambapo uchunguzi kuhusu kesi ya Noos uliendeshwa.

Infante Cristina anafuatiliwa katika kesi ya matumizi mabaya ya pesa za umma. Ubadhirifu unaoihusu kampuni ya kihisani ya Noos, ambayo ilikua ikisimamiwa na mumewe, Iñaki Urdangarin.

Miaka minne baada ya kuanzishwa uchunguzi, jaji anayehusika na kesi hiyo, Jose Castro, anaamini kuwa Cristina, ambaye ni binti wa Mfalme Juan Carlos, alishirikiana na mumewe kwa makosa mawili yanayoambatana na kodi.

Ni baada ya uchunguzi uliyoendeshwa kuhusu fedha ziliyotolewa kwa kuudhamini mradi uliyojulikana kama Velodrome Palma de Mallorca, ambapo jaji alijikuta ameangukia mikataba inayotia mashaka ambayo ilitiliwa saini na kampuni ya Noos na jimbo la Valencia, pamoja na visiwa vya Balearic, yaani utoaji wa bili kupitia kampuni inayomilikiwa kwa sehemu moja na Cristina pamoja na mume wake.

Iñaki Urdangarin, alifunguliwa mashitaka mwezi Desemba mwaka 2011 na alipigwa marufuku kuendesha shughuli yoyote rasmi.

Baadae tarehe 3 mwezi Aprili mwaka 2013, Cristina, ambaye anatuhumiwa kushirikiana na mume wake alifunguliwa mashitaka pia. Tangu wakati huo, Mfalme Juan Carlos alimkabidhi madaraka mwanawe Felipe VI. Katika sherehe za kukabidhiwa madaraka Felipe VI mwezi Juni mwaka 2014, Cristina hakualikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.