Pata taarifa kuu
Marekani, Ufaransa, Uingereza, IS

Mkutano wa muungano wa kimataifa dhidi ya IS

Mkutano wa muungano wa kimataifa unaondesha vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu linaloshikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria, unafanyika tangu asubuhi Alhamisi Januari 22.

Moja ya malengo yamuungano ni kutathimini hali ya mashambulizi dhidi ya IS  kama hapa kwenye picha, katika mji wa Kobane nchiniSyria Oktoba 10 mwaka 2014.
Moja ya malengo yamuungano ni kutathimini hali ya mashambulizi dhidi ya IS kama hapa kwenye picha, katika mji wa Kobane nchiniSyria Oktoba 10 mwaka 2014. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri kadhaa wa mambo ya kigeni kama Marekani John Kerry na Ufaransa Laurent Fabius wamejielekeza mjini London, nchini Uingereza. Mashambulizi ya muungano dhidi ya kundi la Dola la wapiganaji wa Kiislamu yalianza mwezi Agosti mwaka jana nchini Iraq na kuenea nchini Syria mwezi uliyofuata.

Kwa mujibu wa viongozi wa Uingereza, zaidi ya nchi ishirini zimewakiliswa mapema leo Alhamisi katika mji mkuu wa Uingereza, London. Marekani, Uingereza, Ufaransa, na nchi za Kiarabu zinazoshirikiana katika vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislam.

Nchi hizo za Kiarabu ni Umoja wa falme zakiarabu, Saudi Arabia, Bahrain na Jordan. Mwanajeshi mmoja na rubani mmoja wote kutoka majeshi ya muungano walikamatwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Mjini London, leo asubuhi, wawakilishi kutoka mataifa wanachama wa mmungano unaoongozwa na Marekani wanaoshiriki mkutano huo wameangazia mashambulizi yanayoendeshwa dhidi ya wanajihadi.

Zaidi ya mabomu 5,000 walirushwa katika maeneo yanayo dhibitiwa na wanajihadi nchini Iraq na Syria, kulingana na takwimu ziliyotolewa na Pentagon. Katika mkutano huu, itakuwa pia suala la wapiganaji wa kigeni kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Suala la mashirika yanayofadhili kundi hilo litakua katika ajenda katika ya mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.