Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-SIASA

Sarkozy akosoa mwenendo wa serikali ya Ufaransa

Akionekana kimya tangu mashambulizi yaliyogharimu maisha ya watu 17 katika mji wa Paris, nchini Ufaransa, rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameonekana Jumatano Januari 21 kwenye televisheni France 2 akikosoa vikali mwenendo wa serikali ya Ufaransa.

Nicolas Sarkozy apinga matumizi ya neno " ubaguzi wa rangi" ilililotamkwa na Waziri Mkuu Manuel Valls.
Nicolas Sarkozy apinga matumizi ya neno " ubaguzi wa rangi" ilililotamkwa na Waziri Mkuu Manuel Valls. France2/Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Katika Bunge, upinzani umeendelea kukata tamaa, kutokana na hatua zilizochukuliwa kwa kukabiliana na ugaidi nchini Ufaransa.

Baada ya ukimya uliyotokana na kipindi cha maombolezo ya kitaifa kufuatia kuuawa kwa raia wa Ufaransa katika mashambulizi yaliyoukumba mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambayo yalifuatiwa na maandamano ya kitafa ya kulaani mashambulizi hayo, Nicolas Sarkozy jana Jumatano alijaribu kuikosoa serikali, akibaini kwamba mwenendo iliyochukua hautaleta manufaa kwa usalama wa raia wa Ufaransa.

Akikosoa matumizi ya neno "ubaguzi wa rangi" lililotamkwa na Waziri mkuu Manuel Valls, akielezea hali inayojiri katika baadhi ya maeneo ya Ufaransa, Sarkozy amesema mtu kama kiongozi mkuu wa srikali hapaswi kutumia neno hilo.

" Ni kosa", amesema kiongozi wa sasa wa chama cha UMP, ambae, bila kuhatarisha umoja wa kitaifa ambao bado unaripotiwa katika jamii ya wanasiasa, ameweka wazi utaratibu ambao unaweza kutumiwa kwa kuepusha kufunjika kwa umoja wa kitaifa.

Kama kujibu " kwa haraka ", dhidi ya tishio hili la kigaidi ambalo limeonekana kushika kasi "kubwa mno", mazungumzo baina ya raia wote wa Ufaransa yanapaswa kuendelea, ameendelea kusema Nicolas Sarkozy.

" Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha aibu, ambacho kati ya mwaka 1948 na 1994, kiliwabagua watu kutokana na maumbile yao kati ya weusi na wazungu nchini Afrika Kusini. Kulinganisha Jamhuri ya Ufaransa kwa ubaguzi wa rangi, ni ni kosa kubwa", amekosoa Nicola Sarkozy.

Wakati huohuo, Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls, amejitetea usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Januari 22, baada ya ukosoaji wa Nicolas Sarkozy, akibaini kwamba pendekezo la Sarkozy halina umuhimu wowote kwa usalama wa Ufaransa dhidi ya ugaidi.

" Sarkozy anajua kwamba pendekezo lake halikubaliki na serikali ya Kisoshalisti, ambayo ilimaliza mapema muda wa miaka mitano wakati ambapo hatua hii ilianza wakati wa utawala wake. Kwa kifupi, kiongozi wa upinzani anarejea katika ukumbi wa siasa, na umoja wa kitaifa ulikuwepo bila shaka", amesema Manuel Valls.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.