Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-DIPLOMASIA

Wabunge na Maseneta wa Ufaransa ziarani Damascus, Valls na Hollande wajibu

Wabunge wawili na Maseneta wawili wa Ufaransa kutoka mrengo wa kushoto na kulia, walijielekeza Syria Jumatano wiki hii kukutana kwa mazungumzo na rais wa Syria Bashar al Assad.

Rais wa Syria Bashar al Assad akiwapokea ujumbe wa Bunge la Ufaransa Jumatano Februari 25 mjini Damas.
Rais wa Syria Bashar al Assad akiwapokea ujumbe wa Bunge la Ufaransa Jumatano Februari 25 mjini Damas. REUTERS/SANA/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 pamoja na kufungwa kwa ubalozi wa Ufaransa Damascus, wawakilishi wa raia wa Ufaransa wanajielekeza nchini Syria.

Kwa upande wa Syria wanaona ziara hii ni ushindi katika masuala ya kidiplomasia. Lakini Waziri mkuu Manuel Valls na rais François Hollande bado wanasita kueleza kuwa ni jitihada za kufufua uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, ambazo uhusiano wao umeendelea kudorora kwa miaka mitatu sasa.

Iwe rasmi au kibinafsi, ziara hii ya ujumbe wa Ufaransa mjini Damascus inafungua njia katika siasa za kutengwa kwa rais Bashar al Assad, ambayo ilichukuliwa na serikali ya Ufaransa tangu miaka miitatu iliyopita.

Vyombo vya habari vya umma nchini Syria vimeonyesha ziara hii kama ushindi wa kidiplomasia wa Damascus, na vimejitahidi kuonyesha picha ya kisiasa na usalama kupitia ziara hii, ameeleza mwandishi wa RFI, Beyrut, Paul Khalifeh.

Kwenye ukurasa wa Facebook wa Ikulu ya rais wa Syria imebaini kwamba ujumbe huo ulikua unaundwa, mbali na wabunge wa Masaneta, na “ mkaguzi mkuu” wa wizara ya ulinzi ya Ufaransa na mshauri wa usalama kwenye ubalozi wa Ufaransa Beyrut.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.