Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-UHISPANIA-AJALI-USALAMA

Airbus A320 : Hollande, Merkel na Rajoy kwenye eneo la tukio

Operesheni kubwa imerudi kufanyika Jumatano wiki hii katika mlima wa Alpes kusini mwa Ufaransa, katika jaribio la kupata miili 150 ya watu waliofariki katika ajali ya Airbus A320 ya shirika la ndege la Ujerumani la Germanwings iliyoanguka Jumanne wiki hii.

Angela Merkel, François Hollande na Mariano Rajoy wakiwasili kwenye eneo la tukio katika mlima wa Alpes, Jumatano Machi 25 mwaka 2015.
Angela Merkel, François Hollande na Mariano Rajoy wakiwasili kwenye eneo la tukio katika mlima wa Alpes, Jumatano Machi 25 mwaka 2015. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kisanduku cheusi cha kurekodi mawasiliano katika ndege kiliyookotwa kimeanza kufanyiwa uchunguzi mjini Paris, nchini Ufaransa na matokeo ya awali yalikua yanatazamiwa kutolewa alaasiri Jumatano wiki hii.

Rais wa Ufaransa François Hollande, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy wamewasili kwenye eneo la tukio.

Viongozi hao wamekutana na madaktari, maafisa wa Idara ya huduma za dharura na wanajeshi ambao wanaendelea na zoezi la kutafuta miili ya wahanga. Miili ya raia wawili kutoka Uhispania imetambuliwa miongoni mwa abiria.

Kisanduku hicho cha sauti kiliyopatikana ni kile kinachorekodi sauti ya marubani na maafisa wanaowasiliana nao kwenye viwanja vya ndege. Licha ya kuwa kisanduku hiki kimeharibika, kimesafirishwa mapema asubuhi Jumatano wiki hii kwenye Ofisi ya Uchunguzi na Uchambuzi (BEA) mjini Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.