Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Kamati maalumu ya majadiliano yafanyiwa mabadiliko

Serikali mpya ya mrengo wa kushoto nchini Ugiriki, leo Jumatatu imetangaza kufanya mabadiliko kwenye kamati yake maalumu ya majadiliano kuhusu deni lake.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, Machi 20, Brussels.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, Machi 20, Brussels. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linatolewa wakati huu mazungumzo yao na Umoja wa Ulaya, shirika la fedha duniani IMF na wakopeshaji yakiwa hayajapiga hatua kubwa katika kipindi cha miezi 2 iliyopita.

Taarifa ya Serikali imesema kuwa timu ya wapatanishi wa kisiasa itaundwa chini ya waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Euclid Tsakalotos ambaye amebobea kwenye masuala ya uchumi na atakuwa na jukumu la kusimamia mazungumzo mapya.

Nchi ya Ugiriki imeendelea kujaribu kuwasahwishi wakopeshaji wa nchi yake ili waruhusu kutolewa kwa kiasi cha euro bilioni 7.2 kilichosalia kama sehemu ya mkopo wake iliyopewa na Umoja wa Ulaya pamoja na IMF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.