Pata taarifa kuu
POLAND-UCHAGUZI-SIASA

Poland: Andrzej Duda achaguliwa kuwa rais

Kwa mujibu wa tafiti ziliofanywa baada ya matokeo uchaguzi Jumapili jioni nchini Poland, Andrzej Duda kutoka chama cha Conservative ameshinda uchaguzi wa rais na asilimia 52 ya kura. Duda amemshinda rais anayemaliza muda wake kutoka chama cha meno wa Kati wa kulia, Bronislaw Komorowski, ambaye amekubali kushindwa na kupata asilimia 48 ya kura.

Andrzej Duda alifanya ishara ya ushindi baada ya matokeo ya kwanza ya raundi ya pili ya uchaguzi wa rais katika Warsaw, Mei 24
Andrzej Duda alifanya ishara ya ushindi baada ya matokeo ya kwanza ya raundi ya pili ya uchaguzi wa rais katika Warsaw, Mei 24 REUTERS/Kacper Pempel
Matangazo ya kibiashara

Baada ya saa moja na nusu ya kuchelewa kutokana na kifo cha raia mmoja katika kituo cha kupigia kura, matokeo ya uchaguzi yalitangazwa. Asilimia 52 ya kura dhidi ya asilimia 48: katika makao makuu ya Andrzej Duda, watu wamejawa na furaha, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Warsaw, Damien Simonart.

Rais mpya aliyechaguliwa amepitia umati hadi kufikia mimbari. Andrzej Duda almewahutubia wafuasi wake akianza kumpongeza mshindani wake. " Namshukuru rais Bronislaw Komorowski kwa ajili ya ushindani wetu wakati wa kampeni za uchaguzi na kwa pongezi aliyonipa", amesema Duda.

Akiungwa mkono na Kanisa za Poland, ambazo pia zimempongeza kuchaguliwa kwake, Andrzej Duda ana msimamo wa mkali kihafidhina katika masuala kama utoaji mimba, katika kurutubisha vitro na utambuzi wa wanandoa wenye jinsia moja.

" Milango ya Ikulu itakuwa wazi kwa jitiahada za kijamii ambazo nakubaliana nazo kwa kuziwekea mashaka au kutokubaliana nazo. Ninawaahidi: yote tutayafanya kwa uwazi", amesema Dudu, rais mteule wa Poland.

Zoezi la kukabidhiana madaraka litafanyika mwezi Agosti, lakini mapambano kwa uchaguzi wa wabunge umeanza. Baada ya ushindi wa Duda, wafuasui kutoka chama cha Conservative wana matumaini ya kupata mamlaka kamili nchini Poland. Hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.