Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: kampeni ya "ndiyo" au "hapana" imeaza Athens

Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, ameahidi Jumatano wiki hii kwamba kura ya maoni ya Jumapili Julai 5 kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wakopeshaji wa Ugiriki, bila shaka itakua.

Wafuasi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni, mbele ya Bunge la Ugiriki katika mji wa Athens, Jumatatu 29 Juni.
Wafuasi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni, mbele ya Bunge la Ugiriki katika mji wa Athens, Jumatatu 29 Juni. REUTERS/Neil Hall
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Ulaya limekosoa vikali kufanyika kwa kura hiyo ya maoni likiitaja kuwa haieleweki. Raia wa Ugiriki hawajaelewa kinachoendelea, Jambo ambalo halikuzuia kampeni ya “ndio” au “hapana” kuanza.

Mabango yanayowatolea wito raia kupiga kura ya “hapana” Jumapili ijayo yaliyotundikwa na chama cha Syriza kwenye kuta za nymba katika mitaa ya mji wa Athens.

Kwa upande wake upinzani wa mengo wa kati-kulia umekua ukitumia runinga kwa kumdhihaki waziri mkuu, Alexis Tsipras, na kukosoa ahadi ambazo hatekelezi, hususan kuhusu kufungwa kwa mabenki. Lakini mjadala ni mkali katika mitaa na katika familia mbalimbali, amabazo zinaishi kila siku bila kuwa na matumaini zaidi.

Kambi inayounga mkono kura ya “ndiyo” imeendelea kujidhatiti hivi karibuni katika uchaguzi kwa hofu inayohusiana na hali ya mabenki.

Kambi inayounga mkono kura ya “hapana” inaelewa mrengo wa kushoto wenye itikadi kali, mrengo wa kushoto, mrengo wa kulia na sehemu kubwa ya raia ambao wameathirika na hali hii ya mabenki, huku wakichukulia madai mapya ya wakopeshaji kama nia ya kuifedhehesha Ugiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.