Pata taarifa kuu
UFARANSA-UPELELEZI-USALAMA

Ufaransa: Sheria kuhusu upelelezi yazingatia Katiba

Baraza la Katiba nchini Ufaransa limesahihisha Alhamisi jioni wiki hii mlolongo wa sheria kuhusu upelelezi, lakini Ibara tatu zimefutiliwa mbali. Sheria hii imekua ikikosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu na hasa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambayoalhamisi wiki hii ilioelezea wasiwasi.

Makao makuu ya DGSI, Idara ya ujasusi ya Ufaransa, katika mji wa Levallois-Perret katika jimbo la Hauts-de-seine, karibu na Paris.
Makao makuu ya DGSI, Idara ya ujasusi ya Ufaransa, katika mji wa Levallois-Perret katika jimbo la Hauts-de-seine, karibu na Paris. Creative Commons/NemesisIII
Matangazo ya kibiashara

Uanzishwaji wa "masanduku meusi" miongoni mwa makampuni yanayotoa huduma za intaneti, ambayo yametakiwa kuwa yakirekodi mawasiliano ya kila mmoja. Kulingana na maamuzi ya wazee wa Baraza la Katiba, uamzi huo sio ukiukwaji wa uhuru wa raia kama inavyoelezwa na Katiba.

Makampuni ya kutoa huduma za intaneti na mawasiliano mengine yametakiwa kutumia zana zenye nguvu kwa ajili ya uchunguzi wa mawasiliano, kama vile IMSI-catcher, masanduku yenye uwezo wa kurekodi mazungumzo na kubadilishana data zote katika ya umbali wa zaidi ya mita mia moja. Hapa tena, Baraza la Katiba hakioni ubaya wowote katika suala hili.
Baadhi ya Ibara zinazokiuka na kuvunja haki za binadamu zimefutiliwa mbali

Umoja wa Mataifa watiwa wasiwasi

Hata hivyo nakala ya sheria hii ilizua mvutano mkali, ikiwa nchini Ufaransa na katika nyanja ya kimataifa. Umoja wa Mataifa inatiwa wasiwasi na sheria hii kuhusu upelelezi ambayo imepitishwa na Bunge la Ufaransa, amearifu mwandishi wa RFI mjini Geneva, Laurent Mossu. Kamati ya haki za binadamu iliokutana mjini Geneva imekosoa vikali sheria hiyo katika ripoti iliyotolewa Alhamisi kufuatia uchunguzi ulioendeshwa na wataalamu 18 wanaojitegemea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.