Pata taarifa kuu
UINGEREZA-WAHAMIAJI-SHERIA-HAKI

Wahamiaji wazidisha majaribio ya kuingia Uingereza

Wahamiaji haramu wamezidisha majaribio ya kuingia nchini Uingereza wakitokea katika mji wa Calais, Kasakazini mwa Ufaransa wakipitia katika barabara za ardhini, ambazo wanaona kuwa ndio njia ya ziada kwao ili waweze kuingia nchini humo.

Polisi ikijaribu bila mafanikio kuwakamata wahamiaji wanaojaribu kupita kwenye eneo la barabara za ardhini katika mji wa Calais Jumatano Julai 29.
Polisi ikijaribu bila mafanikio kuwakamata wahamiaji wanaojaribu kupita kwenye eneo la barabara za ardhini katika mji wa Calais Jumatano Julai 29. AFP PHOTO / PHILIPPE HUGUEN
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wahamiaji hao hawarahisishiwi na polisi ya Uingereza, polisi ya nchi hiyo inakabiliana na muhamiaji yeyote atakaye penya na kuingia nchini uingereza.

Kwa sasa mchezo wa panya na paka umeendelea kushuhudiwa nchini humo kufuatia jaribio hilo.

Jumatano usiku wiki hii, vikosi vya usalama viliwaona wahamiaji haramu 300, kwa mujibu wa chanzo cha polisi, ambacho kimeonesha kuwa kati ya wahamiaji haramu 800 na 1000 waliorodheshwa pembezoni mwa eneo wanakokusanywa.

Kama majaribio ya kuingia nchini Uingereza yanaongezeka, kuna tofauti katika idadi ya wahamiaji wanaokuwepo kila usiku pembezoni mwa eneo wanakokusanywa. Wakati viongozi na mamlaka ya eneo hilo wanakopitia wahamiaji haramu wanabaini kuwa idadi ya wahamiaji hao haramu ni kati ya 1000 na 2000, mashirika na wahamiaji wenyewe wanabaini kuwa idadi yao ni kati ya " 250 hadi 500, ikiwa itazidi ".

Kwa kuwahesabu, polisi inachunguza idadi ya wahamiaji haramu iliofurusha, ameeleza Johann Cavallero, katibu wa kikanda CRS kwa muungano wa vyama vya wafanyakazi. " Lakini, ni kuwa makini, inaweza kuwa kundi moja la watu 10 (...) ambao wamekua wakifanya majaribio 3 au 4, ghafla wanakua wameingi watu 30 ", amesema Johann Cavallero.

Wahamiaji haramu wanatumia mbinu gani kwa kuvuka vizuizi vya polisi?

Mbinu kwa kuvuka vizuizi vya barabarani vya polisi ni rahisi: kukimbia katika pande zote, mara nyingi, na kupiga kelele, mpaka polisi, inazidiwa na idadi, bila kujua ikamate nani iache nani, na hivyo kushindwa kuwadhibiti.

“ Wahamiaji haramu wengi wanatokea Sudan, Eritrea, Somalia, Afghanistan, Syria... idadi kubwa ya wahamiaji 3,000 walioko katika mji wa Calais wanatokea katika nchi zinazokumbwa na mizozo ya kivita, ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji. Hiyo hiyo ni mooja ya sababu zinazopelekea wasifurushwe ", amekumbusha Mwendesha mashitaka wa mji wa Boulogne-sur-Mer, Jean-Pierre Valensi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.