Pata taarifa kuu
TURUK-PKK-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mashambulizi ya Zergele: Ankara yakanusha vifo vya raia

Tangu Julai 24, Uturuki imeendelea kuzishambulia ngome za wapiganaji wa PKK katika mkoa unaojitegemea wa Kurdistan nchini Iraq.

Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015.
Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Mamlaka ya mkoa, raia ni miongoni mwa waathirika. Serikali ya Uturiki ilitangaza Jumamosi Agosti 1 kwamba imeanzisha uchunguzi ili kuthibitisha madai hayo.

Uchunguzi ulioanzishwa Jumapili mwishoni mwa juma hili unaweza kuzaa matunda. Tangu Jumapili, jeshi la Uturuki limekanusha kuwa mashambulizi yake yamewalenga raia, hasa wakati wa mashambulizi ya angani yalioendeshwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi katika kijiji cha Zergele.

Kwa mujibu wa serikali ya Kurdistan nchini Iraq, inasadikiwa kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wanawake wawili ambao walikuwa hawahusiki kwa njia yoyote na wapiganaji wa PKK.

Jeshi Uturuki limebaini kwamba uchunguzi ambao umeanzishwa haujabaini kuwa maeneo yalioshambuliwa yalikua yakikaliwa na raia. "Maeneo yaliolengwa yalichaguliwa na watu wenye taaluma za kutosha kulingana na data ziliothibitishwa, na baada ya uchunguzi wa kina uliofanyiwa mapitio", jeshi la Uturuki limehakikisha Jumapili Agosti 2. Hata hivyo ni vigumu kuamini kwamba mashambulizi haya hayakusababisha vifo vya raia.

Kwa mujibu wa serikali ya Uturuki, wizara ya mambo ya nje ya Uturuki anafanya kazi kwa ushirikianao na serikali ya Kurdistan nchini Iraq ili kujaribu kutoa mwanga juu ya kesi hii. Lakini baada ya taarifa za jeshi la Uturuki Jumapili Agosti, ni vigumu kujua kama kweli uchunguzi huo bado unaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.