Pata taarifa kuu
AUSTRIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Austria: mamia ya wahamiaji njiani kwenda Munich kwa treni

Mamia ya wahamiaji wamefika kwa mara ya kwanza nchini Austria kwa treni Jumatatu alasiri Agosti 31. Mamlaka ya Hungary imekataa kurejesha maelfu ya wahamiaji ambao wamepiga kambi katika vituo yake vya treni.

Wahamiaji wanabadili treni baada ya kuwasili katika mji wa Budapest, wakielekea Ujerumani, Jumatatu, Agosti 31, 2015.
Wahamiaji wanabadili treni baada ya kuwasili katika mji wa Budapest, wakielekea Ujerumani, Jumatatu, Agosti 31, 2015. AFP PHOTO / PATRICK DOMINGO
Matangazo ya kibiashara

Treni ilisimama muda mfupi, kisha iliendelea na safari yake hadi Munich, Kusini-Mashariki mwa Ujerumani, ambapo wahamiaji wanataka wote kwenda baada ya kauli nzuri ya Angela Merkel juu.

Wakati treni inaingia kituo hicho, hakuna mhamiaji au kitu chochote kiliruhusiwa kutoka nje. Polisi ya Austria imekua ikisaidia abiria wa Hungary na Austria pamoja na watalii kutoka nje ya mabehewa. Kati yao, msichana ambaye mara kwa mara husafiri kati ya Budapest na Vienna. Msichana huyo anafanya kazi sehemu hiyo katika katika kituo kikuuu cha treni, ambako anauza dukani.

Alikuwa tayari amekaa katika treni na mwenzake wakati aliona mamia ya wahamiaji wakijaribu, ghafla kulirudi pia kuingia katika treni, msichana huyo alimuelezea mwandishi wetu katika mji wa Vienna, Blaise Gauquelin. Inakadiriwa kuwa 95% kati ya wahamiaji hao walikuwa wa kiume, wenye umri wa chini ya miaka 30.

" Kisha tulianza safari yetu, lakini tulizuiliwa karibu masaa manne kwenye mpaka kati ya Hungary na Austria. Hakuna mtu aliyetushughulikia, ilikua tu vurugu! Wahamiaji walikuwa wakijaribu kututisha ili tusiweze kusema chochote na tulikuwa peke yetu, hakuna mtu alikuja, polisi ya Hungary haikuja mara moja, mpaka tulivyofika mjini Vienna ", amesema msichana huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.