Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALAYASIA-USAALAMA WA ANGA

Bawa la ndege lililopatikana katika kisiwa cha Réunion ni la MH370

Vyombo vya sheria vya Ufaransa vimethibitisha Alhamisi wiki hii, mwezi mmoja baada ya viongozi wa Malaysia, kwamba kipande cha bawa la ndege kiliopatikana mwishoni mwa mwezi Julai, katika kisiwa cha Réunion " kwa uhakika " ni cha Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliyotoweka mwezi Machi mwaka 2014.

Askari polisi wa Ufaransa wakikagua kipande cha bawa la ndege kiliyopatikana kwenye pwani ya kisiwa cha Réunion, Juni 29, 2015.
Askari polisi wa Ufaransa wakikagua kipande cha bawa la ndege kiliyopatikana kwenye pwani ya kisiwa cha Réunion, Juni 29, 2015. REUTERS/Zinfos974/Prisca Bigot/Files
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilitoweka na watu 239 wakati ilikua ikifanya safari kati ya nKuala Lumpur na Beijing.

Uchunguzi umepelekea " kuthibitisha kwa uhakika kwamba kipande cha bawa la ndege kiliyogunduliwa katika kisiwa cha Réunion ni kile cha ndege chapa MH370 ", Ofisi ya mashataka ya mji wa Paris imebaini. Ofisi hiyo ilianzisha uchunguzi mara baada ya ajali kwa sababu waathirika wanne ni raia wa Ufaransa.

Kwa upande wake Marie dozi, mwanasheria wa Ghyslain Wattrelos aliyepoteza mke na watoto zake wawili katika ajali hiyo, " ni ukurasa unaogeuka ", amesema mwanasheria huyo.

" Tathmini zote na uchunguzi wote vinapaswa kuendeshwa kwa bawa hilo, bila shinikizo lolote, ikiwa ni pamoja na viongozi wa Malaysia ", amesema mwanasheria.

Chimbuko la kipande hiki cha bawa la ndege, kiitwacho Flaperon, lilikua mashaka kidogo.

Viongozi wa Malaysia walithibitisha baada ya ugunduzi kipande hiki cha bawa katika pwani ya kisiwa cha Réunion kwamba ni kipande cha Boeing 777. Lakini tangu aina ya ndege hiyo kuanza kufanya kazi mwaka 1995,ndege mbili pekee za aina ya Boeing 777 zilihusika katika ajali mbaya iliyowaua watu wengi. Ajali zote hizo zilitokea mbali kabisa na Bahari ya Hindi.

Kuala Lumpur ilihakikisha Agosti 6 kuwa kipande hicho cha bawa ni kutoka ndege MH370. Ofisi ya mashitaka mjini Paris ilionekana kuwa na tahadhari zaidi, ikisema kuwa " haina ushahidi wa kutosha kuhusu bawa hilo ", ikisubiri kufanyika kwa uchunguzi.

Uchambuzi uliofanyika tangu wakati huo, katika maabara ya Ofisi kuu ya Silaha ya Wizara ya Ulinzi (DGA TA) katikamji wa Balma, karibu na mji wa Toulouse, ulisaidia kupata " namba tatu ziliokua ndani ya flaperon " ambazo zilipelekea shirika liliosaini kandarasi na Boeing, kampuni ya Airbus Defense and Space (ADS-SAU) katika mji wa Seville (kusini mwa Uhispania), mwendesha mashitaka Paris amesema katika taarifa yake.

Baada ya ugunduzi wake, Ufaransa ilianzisha kwa muda wa siku kumi kampeni ya kutafuta ndege hiyoi katika pwani ya kisiwa cha Réunion. Lakini opereshi hizo hazikufanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.