Pata taarifa kuu
UTURUKI-URUSI-USHIRIKIANO-USALAMA

Uturuki yakasirishwa na kitendo cha Urusi

Uturuki kwa mara ya pili imemwagiza Balozi wa Urusi nchini humo baada ya ndege za kivita za nchi yake kupaa katika anga yake bila ya idhini kwenda kutekeleza mashambulizi nchini Syria.

Picha ya ndege ya Urusi katika uwanja mdogo wa ndege katika kambi ya jeshi la Heymim, Syria, iliyotolewa na Wizara ya ulinzi ya Urusi.
Picha ya ndege ya Urusi katika uwanja mdogo wa ndege katika kambi ya jeshi la Heymim, Syria, iliyotolewa na Wizara ya ulinzi ya Urusi. REUTERS/Ministry of Defence of the Russian Federation
Matangazo ya kibiashara

Uturuki inasema Jumapili iliyopita ndege za kivita za Urusi kwa mara nyingine zilipaa katika angaa lake bila ya idhini kutoka kwao.

Jumamosi iliyopita hali kama hii pia ilitokea na kusabbaisha ndege za Uturuki kutua kwa dharura baada ya kukutana na ndege ya Urusi.

Urusi imekiri ni kweli Jumamosi ndege zake zilipaa katika anga la Uturuki bila idhini na kutoa sababu ilikuwa tu kwa sekunde chache kutokana na hali mbaya ya hewa lakini haijazungumzia tena tukio la Jumamosi.

Urusi imeendelea kutekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya waasi na wapiganaji wa Islamic State katika maeneo mbalimbali nchini Syria, uamuzi ambao unakosolewa na Mataifa ya Magharibi.

Marekani inaonya kuwa ikiwa Urusi itaendelea na mashambulizi hayo huenda hali nchini Syria ikaendelea kuwa mbaya.

Muungano wa majeshi ya nchi za Magharibi NATO pia yametaka Urusi kusitisha mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.