Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USALAMA-UGAIDI

Mtuhumiwa mpya ashtakiwa Ubelgiji kwa kuhusika katika mashambulizi ya Paris

Mtuhumiwa mpya amefufunguliwa mashtaka Jumatatu wiki hii nchini Ubelgiji kwa kuhusika katika mashambulizi mjini Paris, siku moja baada ya operesheni kabambe dhidi ya ugaidi, Ofisi ya Mashtaka ya Ubelgiji imetangaza katika taarifa yake.

Askari wa Ubelgiji katika mtaa mmoja jijini Brussels, Novemba 21, 2015.
Askari wa Ubelgiji katika mtaa mmoja jijini Brussels, Novemba 21, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Mtu huyo anashtakiwa kwa kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi na mashambulizi ya kigaidi" mjini Paris, Ofisi ya mashitaka imebaini, na kuongeza kwamba mtuhumiwa amewekwa chini ya ulinzi.

Huyu ni mtu wa nne kushtakiwa nchini Ubelgiji katika uhusiano wa moja kwa moja na mashambulizi ya Novemba 13 katika mji mkuu wa Ufaransa. Mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya zaidi ya watu 130. Kundi la Islamic State lilikiri kuhusika kwa mashambulizi hayo.

Watu wengine kumi na tano waliokamatwa Jumapili usiku katika wilaya kadhaa za mji wa Brussels na Charleroi (kusini) waliachiliwa, Ofisi ya mashtaka imeongeza.

Aidha, kati ya watu watano waliokamatwa Jumatatu nchini Ubelgiji, wawili waliachiliwa. Wengine watatu bado wako kizuizini hadi pale "uchunguzi wa zaida utakapofanyika" kwa mujibu wa Ofisi ya mashtaka ya Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.