Pata taarifa kuu
UINGEREZA-BBC-DEMOKRASIA

Uingereza: serikali yatazamia kuwekeza katika BBC ili kuongeza ushawishi wake

Serikali ya Uingereza imesema Jumatatu wiki hii kuwa itawekeza Paundi milioni 289 (sawa na Euro milioni 412) katika miaka ijayo katika Idara ya kimataifa ya BBC ili kuendeleza maadili ya kidemokrasia na hivyo kusaidia kuboresha usalama.

Nembo ya BBC jijini London, Novemba 12, 2012.
Nembo ya BBC jijini London, Novemba 12, 2012. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Uwekezaji huu katika Idara ya kimataifa ya BBC utafikia Paundi milioni 34 kwa mwaka 2016-2017 (Aprili kwa Aprili) na kisha Paundi milioni 85 kwa mwaka hadi mwaka 2020 ili kuendeleza mfumo wa digital katika Idara mbalimbali, redio na televisheni.

Serikali itachangia kuendeleza Idara ya kimataifa ya BBC nchini Korea Kaskazini, Urusi, Mashariki ya Kati na Afrika.

"Mamilioni yaliotangazwa leo yatasaidia BBC kutekeleza ahadi yake ya kutetea demokrasia kupitia habari sahihi, bila ya upendeleo na kujitegemea", amepongeza Mkurugenzi mkuu wa BBC Tony Hall, ambaye anakabiliwa na changa moto nyingi kwa Idara zake nchini Uingereza.

Kwa serikali, ambayo Jumatatu imetangaza mfululizo wa hatua za kuimarisha uwezo wake wa kijeshi na kujibu tishio la kundi la Islamic State, fedha hizo zitatumika kuendeleza "maadili na maslahi yake duniani kote", sambamba na Idara zake za kidiplomasia na ahadi za fedha kwa ajili ya maendeleo.

BBC inasikilizwa na watu milioni 308 na inalenga watu milioni 500 ifikapo mwaka 2022.

BBC, ilianzishwa mwaka 1932, na inapeperusha matangazo yake kwa lugha 29, lakini tangu mwaka 2006 BBC imefunga Idara 15 za lugha za kigeni kwa sababu ya bajeti kuwa ndogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.