Pata taarifa kuu
TALIBAN-AFGHANISTAN

Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan watekeleza shambulio jijini Kabul

Watu 9 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mtu mmoja kujitoa muhanga katika kituo kimoja cha polisi kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.  

Wanajeshi wa Serikali ya Afghanistan wakilinda moja ya eneo lililoshambuliwa na Taliban hivi karibuni
Wanajeshi wa Serikali ya Afghanistan wakilinda moja ya eneo lililoshambuliwa na Taliban hivi karibuni REUTERS/ Stringer
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili la kujitoa muhanga likilenga kituo kikuu cha polisi mjini Kabul, linatekelezwa ikiwa ni siku chache tu zimepita toka kuanza kwa mazungumzo ya kimataifa kati ya Serikali na wanamgambo wa Taliban.

Wanamgambo wa Taliban wamekiri kuhusika na shambulio hili, huku msemaji wake akidai kuwa limewaua watu zaidi ya 40.

Awali kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya ndani, ilidaiwa kuwa lilikuwa ni shambulio lililotekelezwa kwa kutumia gari, lakini baadae wizara ya mambo ya ndani ilidai kuwa waliojitoa muhanga walikuwa kwa miguu.

Watu 9 wameripotiwa kuuawa ingawa taarifa za vyombo vingine zinadai kuwa ni watu zaidi ya 10 ndio waliouawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya mtu aliyevalia mabomu kujilipua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.