Pata taarifa kuu
SYRIA-GENEVA-UN

Upinzani watishia kususia mazungumzo ya amani kuhusu Syria yanayoendelea mjini Geneva

Mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa ameonya kuhusu uwezekano wa kuvunjika kwa mazungumzo ya amani kuhusu Syria, baada ya upinzani kudai kuwa mashambulizi ya anga yanayoendelea kutekelezwa na Urusi yanaweza kuwaondoa kwenye mazungumzo hayo.

Mpatanishi wa umoja wa mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura
Mpatanishi wa umoja wa mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Muungano mkuu wa upinzani unaoshiriki mazungumzo ya mjini Geneva, unasema kuwa mashambulizi yanayofanywa na Urusi kwenye mji wa Aleppo, ambapo mpaka sasa mabomu zaidi ya 270 yamesharushwa, kunatishia juhudi za wao kuendelea kuwepo kwwenye mazungumzo.

Upinzani huo unataka kabla ya kuendelea na mazungumzo yanayosimamiwa na umoja wa Mataifa, kwanza nchi ya Urusi na vikosi vya Serikali waache mara moja kuendeleza mashambulizi ya anga kwenye miji hiyo.

Kwenye taarifa yao, muungano huo unasema kuwa inshangaza kuona mauaji dhidi ya raia yanaendelea na hakuna mtu yoyote anaesema kitu kuhusu mashambulizi yanaoendelea kufanywa na Urusi.

Kauli ya upinzani inatolewa ikiwa ni siku mbili tu zimepita toka mpatanishi wa mzozo huo, Staffan de Mistura atangaze kuanza kwa mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja kati ya jumbe wa Serikali na ule wa upinzani.

Haa hivyo mpasuko umeanza kushuhudiwa hapo jana ambapo ameonya kuwa hii ni nafasi ya mwisho kwa pande hizo kuafikiana na hatimaye kumaliza machafuko yaliyodumu kwenye taifa hilo miaka mitano iliyopita.

De Mistura, anasema kuwa, ikiwa mazungumzo ya safari hii yatashindikana basi matumaini yote yaliyokuwepo hapo awali kuhusu kufikiwa suluhu yatatoweka.

Mkuu wa ujumbe wa Syria kwenye mazungumzo hayo, balozi Bashar al-Jaafari, amesema kuwa bado kuna tofauti kubwa kati yao na upinzani, kwakuwa wenzao hadi sasa wameshindwa kumtaja ni nani atakayeongoza ujumbe wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.