Pata taarifa kuu
CAMERON-EU-UINGEREZA

Waziri mkuu wa Uingereza atetea bungeni mpango wa mabadiliko uliowasilishwa na rais wa umoja wa Ulaya

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, Jumatano ya wiki hii ametetea mpango wake wa kutaka kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya jumuiya ya umoja wa Ulaya, huku akikabiliwa na upinzani toka kwa wabunge wa upinzani na wale wa ndani ya chama chake

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron REUTERS/Ben Pruchnie
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa mjadala mkali bungeni, waziri mkuu Cameron amewataka wabunge wenzake kusimama pamoja na yeye wakati huu akitarajia pia kukumbana na upinzani mkali toka kwa wabunge wa chama chake cha Conservative na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekosoa mapendekezo mapya.

Cameron amewataka wabunge kupigana pamoja katika kuhakikisha mpango huu unaidhinishwa na nchi wanachama baada ya rais wa umoja wa Ulaya, Donald Tusk kuwasilisha mapendekezo mapya ya mabadiliko ambayo sasa yanasubiri kujadiliwa na nchi wanachama.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron REUTERS/Carl Court/Pool

Hatua hizi zinazochukuliwa sasa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha nchi ya Uingereza haiwi taifa lwa kwanza kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya wakati ikisubiri kufanya kura ya maoni kuamua hatma yao mwaka 2017.

Ndani ya mpango wenyewe unataka kuwepo kwa kipindi cha miaka minne cha dharura kwaajili ya kufanywa malipo ya wafanyakazi wahamiaji, ulinzi kwa nchi ambazo hazitumii sarafu ya Euro na mfumo wa kadi nyekundu ambao unaupa mamlaka makubwa zaidi bunge la Ulaya.

Kwenye utetezi wake waziri mkuu Cameron amewaambia wabunge kuwa mapendekezo haya mapya ni mpango wa mabadiliko ambao utakuwa na manufaa kwa nchi yao na nchi zote za ukanda wa Euro.

Cameron amesema kuwa kutokana na mapendekezo haya mapya ni wazi yanatoa taswira ya baadae ya nchi yao ndani ya umoja wa Ulaya, na kwamba utasaidia kwa sehemu kubwa kufikia maamuzi wakati wa kura ya maoni.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema kuwa huenda mapendekezo haya yakapata upinzani mkali toka kwa baadhi ya nchi ambazo zinapinga matakwa ya Uingereza ndani ya umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.