Pata taarifa kuu
MAREKANI-COSBY

Jaji wa mahakama moja chini Marekani aruhusu kushtakiwa kwa mchekeshaji Bill Cosby

Jaji wa mahakama kuu nchini Marekani ametoa uamuzi na kuruhu kuendelea kwa kesi ya udhalilishaji wa kingono inayomkabili muigizaji na mchekeshaji wa televisheni, Bill Cosby, akitupilia mbali kesi ya mawakili wa utetezi walioomba kesi hiyo ifutwe. 

Muigizaji maarufu wa vipindi vya vichekesho, Bill Cosby
Muigizaji maarufu wa vipindi vya vichekesho, Bill Cosby REUTERS/Eric Thayer/Files
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya wanawake wamejitokeza na kumtuhumu mchekeshaji wa televisheni mkongwe Bill Cosby mwenye umri wa miaka 78 hivi sasa, kwenye madai ambayo yamedumu kwa miongo kadhaa, mengi kati ya hayo muda wake umeshapita kufunguliwa mashtaka.

Mchekeshaji huyo maarufu sana nchini Marekani, alitumia muda wa siku mbili kuhudhuria kesi hiyo kwenye mji wa Norristown, nje kidogo na mji wa Philadelphia, ambapo mawakili wake wanahoji uhalali wa mashtaka yenyewe.

Muigizaji maarufu wa vipindi vya vichekesho, Bill Cosby
Muigizaji maarufu wa vipindi vya vichekesho, Bill Cosby REUTERS/Lucas Jackson/Files

Mawakili wake wanasema kesi nyingi za mwaka 2004 zilitatuliwa kwa kesi ya kiraia mwaka 2006 na hivyo kumuondolea hatia mteja wao dhidi ya makosa yoyote.

Kwenye kesi iliyoisha kwa makubaliano mwaka 2006, Cosby amekiri kuwa ni kweli alimpa kidonge cha usingizi mshichana Andrea Constand na kusisitiza kuwa uhusiano wao ulikuwa wa kawaida na kumtuhumu mwanamke huyo kwa kudanganya.

Mwendesha mashtaka kwenye mji wa Montegomery alifungua kesi hizi mwaka uliopita, akidai kuwa kuna ushahidi mpya uliowasilishwa mwezi July ambapo Cosby alipewa dhamana ya dola za Marekani milioni 1, December 30 mwaka jana.

Upande wa utetezi unasema kuwa kumekiukwa makubaliano ya mwaka 2005 ambayo yalielekeza kuwa mchekeshaji huyo hatafunguliwa mashtaka mengine yoyote na Constand aliyekuwa mwajiriwa chuo kikuu Temple mjini Philadelphia.

Ikiwa Cosby atapatikana na hatua anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela na faini ya dola za Marekani elfu 25.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.