Pata taarifa kuu
UN-EU-MAN-UKIMBIZI

Ban Ki-moon alaani vikwazo dhidi ya wahamiaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani ongezeko la sera za kuwazuia wakimbizi kufika katika mataifa ya Ulaya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alihutubia Bunge la Austria tarehe 28 Aprili, akijibu sera ya kuzuia wimbi la wahamiaji katika nchi hii.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alihutubia Bunge la Austria tarehe 28 Aprili, akijibu sera ya kuzuia wimbi la wahamiaji katika nchi hii. REUTERS/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika Bunge la Austria, Moon ameyataka mataifa ya Ulaya kuheshimu majukumu yao ya Kimataifa ya kuwakaribisha wakimbizi.

Kauli hii inakuja baada ya wabunge nchini Austria kupitisha sheria ya kuwazuia wahamiaji wanaokimbilia nchini humo hasa wale wanaotokea katika mataifa kama Syria yanayoendelea kushuhudia vita.

Katika hotuba aliyoitoa mbele ya Bunge la Austria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa "wasiwasi" na kupitishwa kwa sera ya Ulaya "inayowabana zaidi" wahamiaji.

Mbele ya wabungewakiwepo Rais anayemaliza muda wake Heinz Fischer na wagombea wawili wa wanaotaka kumrithi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hakuficha msimamo wake:

"Mimi nina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa raia wageni hapa na mahali pengine. Viongozi wote wa Ulaya wanapaswa kukumbuka kanuni zilizokongoza bara hili. Mgawanyiko na ubaguzi vinawaumiza watu na kudhoofisha usalama," Ban Ki-moon amelaumu siku moja baada ya serikali ya Vienna kuongeza ugumu katika sheria zake za kutoa hifadhi kwa raia wa kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.