Pata taarifa kuu
ITALIA-SHERIA

Italia: nahodha wa zamani wa meli ya Concordia kusikilizwa

Kesi ya Francesco Schettino, nahodha wa zamani wa meli ya Costa Concordia iliyozama katika pwani ya Italia mwezi Januari 2012 na kusababisha vifo vya watu 32, inafunguliwa Alhamisi hii katika mahakama ya rufaa nchini humo.

Ajali ya meli ya Costa Concordia iliyosababisha vifo vya watu 32 katika pwani ya Italia.
Ajali ya meli ya Costa Concordia iliyosababisha vifo vya watu 32 katika pwani ya Italia. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Francesco Schettino ambaye vyombo vya habari nchini Italia viliomuita kwa jina la utani "Nahodha mwoga" alihukumiwa mwaka jana hadi miaka 16 jela katika mahakama ya mwanzo.

Kikao cha kwanza cha kesi hii mpya kitaanza mapema asubuhi katika mahakama ya rufaa mjini Florence (Tuscane), bila kuwepo kwa Schettino.

Mahakama itatathmini katika kikao hiki cha kiufundi malalamiko ya upande wa wanyonge, vile vile mashitaka dhidi ya mtuhumiwa. kwa Mwezi Mei, vikao kumi na moja tayari vimepangwa.

Francesco Schettino amesema hawezi kuhudhuria vikao vilivyopangwa kwa "sababu binafsi".

"Kama majaji wataona ni muhimu mimi kuhudhuria vikao hivyo na kusikilizwa kwa mara nyingine, basi ntafanya hivyo," Schettino amsema katika barua yake alioandika.

Februari 11, 2015, Mahakama ya Grosseto (Tuscane) ilimuhukumu Francesco Schettino kifungo cha miaka 16 jela kwa kosa la mauaji bila kukusudia,kutelekeza meli na watoto au katika hali ya mazingira tata.

Haraka baada ya hukumu hiyo kutangazwa,wanasheri awa Schettino walikata rufaa.

Wakati huo huo Mwendesha mashitaka wa Grosseto pia alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, akisema kuwa hukumu iliyotangazwa haina nguvu ya kutosha na kuomba ahukumiwe kifungo cha miaka 26 jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.