Pata taarifa kuu
EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

EU mbioni kutoa msamaha wa viza kwa raia wa Uturuki

Brussels inatarajiwa kupiga kura Jumatano hii katika neema ya msamaha wa viza, kwa raia wa Uturuki wanaosafiri Ulaya, ambapo Ankara imekua ikitoa sharti kwa kuendelea kutekeleza mkataba wake uhusuo uhamiaji pamoja na Umoja wa Ulaya lakini unaoziweka nchi za Ulaya katika matatizo.

Meli ya walinzi wa pwani ya Uturuki ikipiga doria katika bahari ya Aegean, Aprili 20, 2016.
Meli ya walinzi wa pwani ya Uturuki ikipiga doria katika bahari ya Aegean, Aprili 20, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Uturuki ilitoa shinikizo juu ya suala hili, na kutishia kuhatarisha mkataba wake wa Machi 18 pamoja na Umoja, ambao unaeleza kuwarejesha nchini Uturuki wahamiaji wapya wanaowasili katika visiwa vya Ugiriki, ikiwa ni pamoja na wanaotafuta hifadhi.

Pamoja na kufungwa kwa barabara ya nchi za Balkan, mkataba umepungua kwa kiasi kikubwa shinikizo kwa Umoja wa Ulaya, kwa kupunguza idadi ya wahamiaji kuwasili kila siku katika visiwa vya Ugiriki kutoka pwani ya Uturuki.

Hivyo hofu imeenea katika Umoja wa Ulaya kwamba Brussels inatakiwa kupunguza vikwazo dhidi ya Uturuki, ambayo inashtumiwa kutoheshimu uhuru wa kujieleza na wakati ambapo shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linaishtumu kuwarejesha makwao kwa nguvu raia wa Syria, ambayo inakumbwa na vita tangu mwaka 2011.

Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, na Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, "kukaribishwa kushuka kwa idadi ya wahamiaji wanaovuka Bahari ya Aegean", wakati wa mazungumzo ya simu Jumanne hii, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la ANATOLIA, na kuongeza kwamba "walijadili" swala la viza.

- Chini ya asharti -

Jumatano, kwa mujibu wa chanzo cha Umoja wa Ulaya, Tume ya Umoja huo inatazamiwa "kuwasilisha muswada wa kuiweka Uturuki kwenye orodha ya nchi zilizopewa msamaha wa viza" kwa muda mfupi (siku 90) katika nchi za ukanda wa Schengen, kwa mfumo wa familia, safari za kibiashara au utalii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.