Pata taarifa kuu
UINGEREZA-ELIZABETH II

Malkia Elizabeth asherehekea siku yake ya kuzaliwa

Sherehe zinaendelea nchini Uingereza siku ambayo Malkia Elizabeth wa pili anapotimiza miaka 90.

Akiambatana na mumewe, Prince Philip, Malkia Elizabeth II ametembelea wafanyakazi wa Ofisi yake.
Akiambatana na mumewe, Prince Philip, Malkia Elizabeth II ametembelea wafanyakazi wa Ofisi yake. REUTERS/Chris Jackson
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu walijipanga katika mitaa ya barabara ya Windsor kumpungia mkono Malkia aliyekuwa juu ya gari la wazi.

Kabla ya hilo, Malkia alikata keki na kukutana na watu wengine waliokuwa na umri kama wake wakionekana wakijadiliana.

Malkia aliwapongeza wale wote waliokuwa wanasherehekea siku ya kuzaliwa ya miaka tisini pamoja naye.

Wabunge nao walipata nafasi ya kumzungumzia na kusema alikuwa ni msingi muhimu kwa taifa lao na nchi za Jumuiya ya Madola.

Waziri Mkuu David Cameron amemwelezea Malkia kama mtu aliyeishi katika vipindi tofauti katika maisha ya raia wengi wa Uingereza.

Huu ni mwaka wake wa 64 katika wadhifa wa Umalkia aliokabhidiwa mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka 26 na ni Malkia wa Uingereza, Canada, Australia, New Zealand na kiongozi wa nchi za Jumuiya ya Madola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.