Pata taarifa kuu
DRC-PAPA WEMBA

Papa Wemba kutunukiwa tuzo la heshima

Jumatatu hii ni siku maalum kwa kutoa heshima ya mwisho kwa gwiji wa Muziki wa Rumba Papa Wemba mjini Kinshasa.

Papa Wemba mgeni wa Alain Pilot kwenye RFI, katika kipindi cha "Bande Passante".
Papa Wemba mgeni wa Alain Pilot kwenye RFI, katika kipindi cha "Bande Passante". © RFI
Matangazo ya kibiashara

Vile vile wakazi wa kijiji cha Molokai wilayani Matonge wanatazamiwa kuupokea mwili wa Papa Wemba kwa kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuzi huyo nguli wa Muziki wa Kiafrika, ambaye alifariki wiki moja iliyopita mjini Abidjan nchini Cote d'Ivoire.

Mwili wake utawekwa sehemu maalum katika kijiji hicho alikozaliwa kwa angalau masaa manne. Papa Wemba pia atatunukiwa tuzo la heshima kama shujaa wa taifa hilo. Rais Joseph Kabila mwenyewe atakua katika jengo la Bunge wakati wa sherehe hiyo.

Siku tatu za kutoa heshima za mwisho kwa Papa Wemba zimeanza Jumatatu hii: sherehe itafanyika katika Bunge, nyingine mapema Jumatatu na usiku kijijini Molokai, nyimbo za Papa Wemba zimeendelea kuchezwa katika kijiji hiki cha Molokai.

Jukwaani na mitaani, kila mtu amekua akiamua kucheza au kuimba chaguo la wimbo "wake" uliopigwa na Papa Wemba. Mmoja wa watoto wa kiroho wa Papa Wemba, Koffi Olomide, aliehojiwa na RFI katika mji wa Kinshasa, amesema amempongeza msanii huyo na kuchagua wimbo wa Mi uliochezwa na papa Wemba.Wiki moja iliyopita katika mahojiano na RFI, nguli wa mwisho wa Muziki wa Rumba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (mwimbaji-mtunzi na mtayarishaji kutoka DRC), Koffi Olomide, alitoa wito kwa mataifa yote ya Afrika kuchagua pamoja siku ya maombolezo kwa heshima ya Papa Wemba.

"Ma Rosa", wimbo uliyochezwa na Papa Wemba katika studio ya RFI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.