Pata taarifa kuu
SUDAN-UN-Machafuko

Vikosi vyenye uhusiano na Serikali ya Sudan vyanyoohewa kidole kwa machafuko yanayoshuhudiwa kwenye jimbo la Darfour

Umoja wa Mataifa UN umelaani vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa dhidi ya vikosi vya kulinda amani na wafanyakazi wa mashirika ya misaada kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan na kudai kuwa hali hiyo haikubaliki. Mkuu wa operesheni ya vikosi vya Kulinda amani kwenye jimbo la darfur nchini Sudan.

Maelfu ya raia waliyoyahama makaazi yao kutokana na machafuko kusini mwa Kordofan wakikimbilia eneo liliyolindwa la Umoja wa Mataifa.
Maelfu ya raia waliyoyahama makaazi yao kutokana na machafuko kusini mwa Kordofan wakikimbilia eneo liliyolindwa la Umoja wa Mataifa. UN
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ibn Chambas amesema kuwa mashamblizi ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kikosi cha dharura cha Serikali RSF hayakubaliki na kwamba wanajeshi hao wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka yao.

Hata hivyo Serikali ya Khartoum imekanusha vikali tuhuma hizi za Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa wao hawaamini kama kweli vikosi hivyo vyenye uhusiano na Serikali vimehusika kwenye machafuko yanyoshuhudiwa kwenye jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Magdi el-Gizouli, wa taasisi ya utafiti “Valley Institute” kuna kundi la wanamgambo linalo jinasibu kwa jina la Rapid Support Forces (RSF) amalo limekua kama jeshi la mamluki, ana linaundwa na watu 6.000.

Kundi hilo imelirejeya hivi karibuni katika mji wa Darfour kushirikiana na jeshi la serikali dhidi ya ya waasi katika jimbo la Kordofan kusini.

Tangu wakti huo, majimbo ya Darfour Kusini na Kaskazini yamekua yalikengwa.

Kwa mujibu wa Ibn Chambaz, watu 200.000 katika mji wa Darfour wameyahama makaazi yao kutokana na machafuko yanayotekelezwa na kundi hilo la wanamgambo toka miezi iliyopita. “Machafuko hayo yanapaswa kusitishwa hata kama wanaungwa mkono”, amesema Ibn Chambas.

Ibn Chambas amewataka waasi wanaoendesha harakati zao dhidi ya serikali, ambao pia wanahusika katika mashambulizi mbalimbali, kusitisha machafuko. “Wameshindwa kukabiliana na jeshi la Sudan, na wamekua tu wakiongeza mateso kwa raia wa Darfour”, amesema Ibn Chambas.

Mshauri wa rais wa Sudan Omar al-Bashir, Ibrahim Ghandour, amekosoa vikali tuhuma za Ibn Chambas dhidi ya wanamgambo kundi la RSF, akibaini kwamba tuhuma hizo si kweli na hazina msingi wowote.

Ibrahim Ghandour, amesema kwamba RSF ni tawi la jeshi la Sudan (SAF), ambalo limekua likikabiliana dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Darfour Kaskazini vijijini. “Kazi yao kubwa ni kupambana na harakati za waasi za kudhibiti miji muhimu katika jimbo la Darfour”, amesema Ibrahim Ghandour.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.