Pata taarifa kuu
SIASA-DEMOKRASIA

Mazungumzo ya kitaifa nchini Gabon: Nchi inaelekea kwenye utawala imara wa rais

Shughuli za mkutano huu wa kitaifa ulioanza Aprili 2, zitakamilika siku ya Jumanne ya wiki ijayo. Tume zimeanza kuwasilisha ripoti zao kwa afisi ya mazungumzo ya kitaifa, ambayo inaandaa kikao kifupi cha mashauriano kwa ajili hiyo. Siku ya Alhamisi, Aprili 25, ilikuwa zamu ya kamati ya kisiasa. Ni vigumu kujua hasa mapendekezo makuu yaliyotolewa na makamishna.

Wajumbe wa tume za mazungumzo ya kitaifa ya Gabon wakiondoka kwenye uwanja wa Urafiki ambapo shughuli za mkutano zinafanyika, Aprili 26, 2024.
Wajumbe wa tume za mazungumzo ya kitaifa ya Gabon wakiondoka kwenye uwanja wa Urafiki ambapo shughuli za mkutano zinafanyika, Aprili 26, 2024. © Yves-Laurent Goma/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Libreville, Yves-Laurent Goma

Mwanakatiba, Telesphore Ondo aliongoza kamati ndogo ya "serikali na taasisi za kisiasa". Wajumbe wa kamati hii ndogo waliidhinisha pendekezo la Gabon la upanuzi wa mamlaka ya Rais wa Jamhuri na Bunge lenye nguvu. "Wananchi wa Gabon wamependekeza kuwa serikali itasimamiwa kikamilifu na Rais wa Jamhuri. Utawala wa rais zaidi ya kile tunachojua hadi sasa. Ndipo wananchi walitaka Bunge liwe na nguvu zaidi, yaani, mamlaka mpya lazima ipewe Bunge. "

Makamishna hao pia walipendekeza Gabon kupitisha Katiba ambayo baadhi ya vipengele, hasa mamlaka ya rais, haviwezi kurekebishwa kwa hiari. "Walitaka Katiba ambayo ni ngumu na kwa hivyo ni ngumu kurekebisha. Wananchi wa Gabon walitaka watendaji, hasa Rais wa Jamhuri, kuwa na muda zaidi wa kutekeleza mipango yake mbalimbali ya kiuchumi na kijamii," anabainisha mtaalamu huyo.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kufungwa kwa kambi ya kijeshi ya jeshi la Ufaransa nchini Gabon, marekebisho ya mikataba ya ulinzi na Ufaransa pamoja na kupunguzwa kwa kiasi kikubwa idadi ya majenerali wapya katika jeshi la Gabon.

Ripoti zote zitapitishwa katika kikao cha mawasilisho siku ya Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.