Pata taarifa kuu

Vatican inafuatilia kwa karibu uchunguzi wa mahakama unaomlenga Kadinali Fridolin Ambongo

Uamuzi wa kufungua kesi za kisheria dhidi ya Kadinali Fridolin Ambongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa "matamshi ya uchochezi" haujaifurahisha Vatican. Askofu Mkuu wa Kinshasa ni mmoja wa washauri wakuu wa Kiongozi wa kanisa Katolika Duniani, Papa Francis, na alimkaribisha papa mkuu wakati wa ziara yake ya kitume mwaka jana.

Kadinali Fridolin Ambongo na Papa Francis mnamo Oktoba 5, 2019.
Kadinali Fridolin Ambongo na Papa Francis mnamo Oktoba 5, 2019. Tiziana FABI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Vatican, Éric Sénanque

Mgogoro wa Kardinali Fridolin Ambongo na vyombo vya sheria vya DRC unafuatiliwa kwa karibu huko Vatican. Askofu Mkuu wa Kinshasa kwa hakika ni mmoja wa watu muhimu wa Papa Francis katika bara la Afrika. Tangu mwaka 2020, amekuwa sehemu ya "C9", baraza hili la makadinali kutoka mabara matano ambao ni washauri wa karibu wa Papa Francis.

Mwanzoni mwa mwezi wa Aprili, mjumbe wa Kongo alipokelewa Vatican, lakini hakuna kilichovuja kutoka kwa mahojiano. Mvutano kati ya Kadinali na mamlaka huko Kinshasa unachukuliwa kwa uzito mkubwa huko Roma, wakati makubaliano ya mfumo wa kuanzisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na makao makuu ya kanisa katoliki, ulitiwa saini huko Vatican mnamo mwaka 2016, na ulianza kutekelezwa miaka miwili iliyopita, baada ya ziara ya Kardinali Parolin, Katibu wa makao makuu ya kanisa Katoliki huko Kinshasa. Kisha alikaribisha "ushirikiano wenye manufaa zaidi wa Kanisa la Kongo na mamlaka ya kiraia". Ushirikiano ambao unakumbana na mkanganyiko katika suala hili la Ambongo, hata kama huko Roma hakuna anayezungumza kwa muda wa kutilia shaka makubaliano haya.

Sio mpya

Mvutano kati ya askofu mkuu wa mji mkuu wa Kinshasa na mamlaka huko Kinsaha sio jambo geni. Katika miaka ya sabini, Kadinali Joseph-Albert Malula alikosoa vikali ubabe wa Jenerali Mobutu huku Kadinali Laurent Monsengwo, mwaka 2011, hakusita kueleza matokeo ya ushindi wa Joseph Kabila katika uchaguzi wa urais kuwa "hayakufuata ukweli au haki.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.