Pata taarifa kuu

Askofu Mkuu Fridolin Ambongo akabiliwa na mashitika kwa matamshi ya uchochezi

Askofu Mkuu wa kanisa katoliki jijini Kinshasa, Fridolin Ambongo, aliye karibu na Papa Francis, anakabiliwa na kesi kuhusu mahubiri yake na mijadala yake muhimu kwa vyombo vya habari juu ya usalama na usimamizi wa kisiasa wa nchi.

Kadinali Fridolin Ambongo Besungu akiondoka baada ya misa ya papa kwenye uwanja wa ndege wa N'Dolo mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Februari 1, 2023.
Kadinali Fridolin Ambongo Besungu akiondoka baada ya misa ya papa kwenye uwanja wa ndege wa N'Dolo mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Februari 1, 2023. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa usiku wa Jumamosi Aprili 27 kuamkia Jumapili Aprili 28 ambapo mwanasheria mkuu wa serikali aliamuru mmoja wa mawakili wawili wakuu wa Kinshasa kuanzisha uchunguzi wa kimahakama dhidi ya kiongozi huyo wa kidini.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Firmin M’Vonde alikuwa tayari ametoa mwaliko kwa Fridolin Ambngo tangu Aprili 22 ambapo kulingana naye, β€œalikataa mwaliko huo”. Jimbo kuu, la kanisa kwa upande wake, linaeleza kwamba mwaliko huu haukuwahi kufika ofisini kwao au kwa Kadinali.

Kwa hivyo mwanasheria mkuu anaamuru kufunguliwa kwa faili ya kisheria dhidi ya askofu mkuu ambaye anaweza kuitwa katika siku zijazo. Anashutumiwa kwa matamshi ya uchochezi yanayojumuisha "uvumi wa uwongo, unaochochea watu kufanya uasi na mashambulizi dhidi ya maisha ya binadamu".

Askofu mkuu, ambae ni miongoni mwa wajumbe wa jopo linalomzunguka Papa Francis, hakusita kushutumu, wakati wa misa ya Pasaka, na kukemea utawala mbaya wa serikali ya FΓ©lix Tshisekedi, akikosoa usimamizi mbaya wa kifedha na usimamizi mbaya wa shida ya usalama. β€œHaki ni tukio la kwanza kukiuka haki za raia wa kawaida na tunatoa hotuba hapa kana kwamba tuna nguvu. Ukweli ni kwamba Kongo haina jeshi,” alitamka, miongoni mwa mambo mengine.

Shirika la habari la Kikatoliki hivi majuzi lilihusishwa na maoni yake ya kuishutumu serikali kwa kuwapa silaha wanamgambo wa Wazalendo na hata waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR mashariki ili kukabiliana na M23. Maoni ambayo yalikataliwa na wakala wa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.