Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Cameroon

Imeshiriki mara 6, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 50 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la Dunia la FIFA.Licha ya kuwa hakuna timu toka barani Afrika ambayo imewahi kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA, timu ya taifa ya Cameroon maarufu kama “ The Indomitable Lions” itakumbukwa kwa yale iliyoyafanya kwenye fainali za mwaka 1982 zilizofanyika nchini Uhispania na kumaliza bila kufungwa kwenye hatua ya makundi. Timu hii pia imeshiriki kwenye michuano ya mwaka 1994, 1998, 2002 na 2010. 

Timu ya taifa ya Cameroon
Timu ya taifa ya Cameroon fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ta taifa ta Cameroon “The Indomitable Lions” iko kwenye kundi A la michuano ya mwaka huu ikijumuishwa pamoja na timu mwenyeji Brazil, Mexico na Croatia.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Timu ya taifa ya Cameroon ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa zikitengeneza wachezaji wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya. Miongoni mwa wachezaji wanaotazamiwa kuleta chachu kwenye timu hii ni pamoja na Benoit Assoiu-Ekotto, Auelien Chediou, Alex Song, Jena Makoun na Stephane Mbia bila kumsahau nahodha Samuel Etoo.

Benchi la Ufundi.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon ni Volker Finke.

Mafanikio kwenye kombe la dunia la FIFA.

Mafanikio pekee ya timu hii ni yale ya mwaka 1990 ambapo Cameroon ilifika kwenye hatua ya robo fainali, kuwa washindi kwenye michuano ya Olympic nchini Sydney mwaka 2000.

Wachezaji waliovuma.

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kuvuma na timu ya taifa ya Cameroon ni pamoja na Riger Milla, Marc-Vivien Foe na Rigobert Song.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.