Pata taarifa kuu
BURUNDI-Sheria

Burundi: wanaharakati wa haki za binadamu waishushia lawama serikali

Mashirika ya kiraia nchini Burundi hii leo yameeleza wasiwasi wao kuhusu kutekeleza majukumu yao kwa uhuru nchini humo, kwa kile wanachodai ni kuendelea kukamatwa kwa wenzao na vyombo vya usalama.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya wanaharakati hawa inakuja kufuatia siku za hivi karibuni, vyombo vya usalama nchini humo kufanya operesheni na kuwakamata wanaharakati ambao wanadaiwa kuwa wakosoaji wakubwa wa serikali ya Burundi.

Wanaharakati hawa wanaitaka Serikali kutotoa vitisho dhidi yao, na kwamba kuwakamata na kuwafunga hakutamaliza tatizo lililopo kwa sasa.

Wakati huo huo vyama vya siasa na Serikali vinakutana hii leo mjini Bujumbura nchini Burundi chini ya usimamizi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo B-NUB, mkutano unaolenga kuboresha maridhiano kati ya wanasiasa na serikali baada ya kuonekana mvutano kati ya pande hizo mbili hivi karibuni.

Raia wakiwa mjini Bujumbura
Raia wakiwa mjini Bujumbura AFP/Esdras Ndikumana

Mkutano huu unafanyika baada ya Umoja wa mataifa kuionya nchi hiyo kuhusu kutumbukia kwenye machafuko ya kisiasa iwapo hakutakuwa na maridhiano ya kisiasa. Huu ni mkutano wa pili kuitishwa na Umoja wa mataifa nchini Burundi katika kipindi cha miezi saba.

Umoja wa mataifa kanda ya maziwa makuu, Uganda, Afrika Kusini na Tanzania walisaidia sana ili taifa hilo litoke katika vita vya wenyewe kwa wenyewe toka viliyodumu mwongo moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.